Thursday, April 17, 2014

MELI YA WATU 400 ILIYOZAMA KOREA YA KUSINI MAWIMBI YAKWAMISHA UOKOZI

Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa baharini imetatiza juhudi za utafutaji na uokoaji wa takriban watu mia tatu baada ya feri ya abiria kuzama katika pwani ya Korea Kusini.
Watu tisa wamethibitishwa kuaga dunia katika mkasa huo.
 
Wengi wa abiria kwenye meli hiyo walikuwa ni wanafunzi wa shule ya upili. Takriban watu mia moja sabini wameokolewa. Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani Heidi C. Agle anashiriki katika operesheni ya uokoaji.
Ameiambia BBC kuwa maandalizi yanafanywa kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho.
Wakati huohuo Rais Park Geun-hye, amewataka waokozi kuharakisha juhudi zao za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Rais Park -- ambaye amejionea meli hiyo mwenyewe, amesema kuwa kila dakika ni muhimu katika kuhakikisha kuwa manusura wanapatikana.
Wapiga mbizi wamekuwa wakikabiliana na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho kilichozama hapo jana.
 
Duru zinasema kuwa meli hiyo ilipoteza mwelekeo huku baadhi ya familia za waathriwa zikihoji mwenendo wa nahodha wa meli.
Hata hivyo nahodha huyo Lee Joon-seok aliomba msamaha na kusema ana majuto tele na kuwa hata hajui la kusema.
Dauru zinseama kuwa miongoni mwa wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa miaka 17 na mwaliamu wao mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi mmoja wa meli hiyo.
Wengine wlaiofariki bado hawajatajwa.
Takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa wtu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287 wakiwa bado hawajapatikana.
 












 


REAL MADRID YATWAA KOMBE LA MFALME..BARCELONA YELEEEEWIII

Timu ya Real Madrid Wamefanikiwa kutwaa kombe la Copa del Rey 2014/2015 .

Madrid waliwacharaza wapinzani wao wa jadi katika ligi ya nyumbani La liga Barcelona mabao 2 kwa 1 katika fainali iliyochezwa jana mbele ya mfalme wa Uhispania .
Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti alikuwa anajikuna kichwa kwani mshambulizi wake nyota Cristiano Ronaldo hakuwa uwanjani kutokana na jeraha la mguu na hivyo ikambidi kumchezesha mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa
zaidi msimu huu Gareth Bale .
Na alidhibitisha udedea wake alipofuma bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tano tu mechi hiyo kukamilika na hivyo kuisadia kutwaa taji lake la 19 la Kombe hilo la mfalme la Copa del rey.
Real Madrid ilidhibitisha niya yao mapema kwa bao la dakika ya 11 Angel Di Maria .

 
 
Bale akishangilia goli la pili lililoipa ubingwa Madrid
 

Modric akioneshana kazi na Iniesta

Lakini ikasawazishwa na bao la Bartra katikadakika ya 68 ya kipindi cha pili.
Bao la ushindi lilifungwa na Gareth Bale dakika tano tu kabla ya mechi hiyo kukamilika .
Bale alitimuka mbio na kumpiku mlinzi wa Barca Marc Bartra katikati ya kiwanja na akafululiza hadi akampiga chenga kipa machachari Jose Manuel Pinto na kuihakikishia Madrid ushindi.
Real Madrid bado iko mbioni kuwania kombe la ligi ya Uhispania, ambapo inashikilia nafasi ya pili na alama 79 alama tatu nyuma ya wakinzani wao Athletico Madrid.
Barcelona ambayo imekuwa ikishuhudia msururu wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika siku za hivi punde inafunga orodha ya tatu bora ikiwa na alama 78.
Madrid sasa inamuda wa kutoka kujiandaa kwa mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich ya Ujerumani.
Mechi nyingine ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya itakuwa kati ya Chelsea ya Uingereza dhidi ya Atletico Madrid.
Nusu fainali hizo zitachezwa juma lijalo.
 
Ubabe na undava kama kawa kama dawa




Mwaka wa shetani..duuu hatuambilii chochote
 
BARCELONA 1-2 MADRID