Wednesday, January 8, 2014

MAN U KICHWA CHA MWENDAWAZIMU YANYOLEWA NA SUNDERLAND

Timu ya soka ya Manchester United ya uingereza imeendeleza wimbi la kupokea vichapo toka kwa vibonde, ambapo siku ya jana ilipokea kichapo cha mbwa mwizi toka kwa vibonde wa ligi kuu ya Uingereza ya Sunderland cha mabao 2-1 katika dimba la Stadium of Light.


Goli la kwanza la Sunderland lilipatikana dk ya 5 likitupiwa kambani na Gadner, na mpaka mapumziko Sunderland walikuwa mbele kwa bao hilo moja.

Katika kipindi cha pili Januzaj aliisawazishia Man Uited katika dk 55 kabla ya Sunderland kupata bao la pili lililotokana na makosa aliyosababishwa na chipukizi wa Man United Januzaj katika harakati za kuondosha hatari langoni mwake na kujikuta akiusundikiza mpira wavuni katika dakika ya 55

Niachie weweeeee..........



 
SUNDERLAND 2-1 MAN UNITED