Wednesday, August 28, 2013

BURUDANI YA LEO-KUKERE DANCE

SIMBA YATAKATA YANGA YAVUTWA SHATI NA COASTAL UNION

Kikosi cha Yanga

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea tena leo, Watani wa wajadi wakishuka katika viwanja tofauti kuwania pointi tatu muhimu. Yanga walikuwa katika dimba kuu la Taifa wakikipiga na Coastal Union ya Tanga,katika mpambano huo timu zote zilitoka sare ya 1-1 baada ya dakika 90 kumalizika.
Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 likitupiwa kambani na Jerryson Tegete na Coastal walijitoa kimasomaso kwa kuchomoa katika dakika ya 16 na Abdi Banda.

Simba walikipiga na JKT Oljoro na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 bao likitupiwa kambani na Chanongo.