Tuesday, August 27, 2013

PATA BURUDANI-VIDEO YA STEVE R&B (RADIO)

MSHINDI WA BIGBROTHER AFRICA 2013 DILISH WA NAMIBIA AKIMWAGA RADHI



Mshindi wa Bigbrother africa 2013 Dilish akioga bila chenga. Dilish kutoka Namibia amefanikiwa kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho kilichodumu kwa siku 90 na kuondoka na kitita cha dola 300,000. usipimee....

Dilish

MAN U CHELSEA ZATOSHANA NGUVU

Man Utd & Chelsea fail to find breakthrough
Rooney akijaribu kumhadaa Lampard katika mtanange huo
Rooney akijaribu kufunga bia mafanikio.

Klabu za Chelsea na Manchester United zimeminyana uwanjani Old Trafford. Pande zote mbili zimekosa kufunga bao, na hivyo kutoka sare ya bila kwa bila.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, wote wamepoteza pointi katika siku kumi na sita za kwanza wa msimu huu, na zinaifuata Manchester City iliyopoteza pointi pia kufuatia mechi dhidi ya Cardiff.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliiambia BBC Sport " Hakuna Upande uliostahili kushinda na kushindwa vile vile, unataka kushinda lakini pande zote zilikua na ulinzi mkali. Na kwa mashabiki najua angalau bao moja lingewafurahisha, iwapo ungekuwa mchuano mzuri''.
Naye meneja wa Manchester United, David Moyes alisema, alivunjika moyo kwa sababu hawakuzoa pointi yoyote, lakini ndivyo ilivyo na hawana budi kujifunza kutokana na hali hiyo.
Chelsea kwa sasa inaongoza ligi kuu kwa pointi saba, ikifuatwa kwa karibu sana na Liverpool na Tottenham, zote zikiwa na pointi sita. Machester United inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi nne.