Wednesday, February 20, 2013

BAYERN YAISULUBU ARSENAL

Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani imeisulubu Arsenal ya Uingereza katika mpambano wa kwanza wa klabu bingwa ya Ulaya katikla dimba la Emirates huku mashabiki wapatao 59,974 wakishuhudia fedheha ya kichapo cha mabao 3-1.

Magoli ya Bayern yalifungwa na Kroos dk 6 kabla Thomas Muller kuongeza la pili dk 20 mpaka mapumziko magbao yalikuwa 2-0. Kipindi cha pili kama Arsenal waliamka vile lakini waaap pamoja na kupata bao la kufutia machozi katika dk 54 lililotupiwa na Podolski kwa kichwa baada ya kipa wa Bayern kufanya makosa katika kudaka mpira wa kona, na dk 76 Mandzukic alipeleka kilio London kwa kutupia kamba ya tatu.


Kroos akifunga goli la kwanza


Muller akitupia la pili

Mandzukic akitupia la tatu

Wilshere na Shwerzteinger

Twendeni tumeshapigwa

Pole mzee wenger unayataka mwenyewe nyoooooo!
ARSENAL 1-3 BAYERN MUNICH