Monday, January 28, 2013

SIMBA, YANGA, AZAM ZAANZA VYEMA DURU LA PILI

MABINGWA watetezi, Simba jana walianza kwa kishindo duru la pili Ligi Kuu Bara kwa kuitungua African Lyon mabao 3-1, katika mechi ambayo kila upande ulikosa kufunga penalti katika kila kipindi.
Ushindi kama huo pia uliandikwa na Azam FC iliyotumia vizuri Uwanja wa Chamazi kuiogesha kipigo Kagera Sugar ya Kagera, kadhalika Coastal Union kule Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo Shooting.

Wachezaji wa Simba wakimnyanyua Ngassa baada ya kufunga goli.

Simba imefikisha pointi 26, lakini ikiendelea kubaki nyuma ya Azam kwa tofauti ya pointi moja, na Yanga inayocheza leo haijaathiriwa na matokeo ya mechi za jana.
Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wachezaji Mrisho Ngassa wa Simba na
Shamte Ally wa Lyon walikosa penalti. Penalti ya Ngassa ingeweza kumpa ‘hat trick’ kama siyo kipa wa Lyon, Abdu Seif kuicheza dakika ya 66 kufuatia Ibrahim Issac kumkwatua Ramadhan ‘Redondo’ Chombo.

Ngassa akiwachachafya mabeki wa African Lyon

Shamte naye alishindwa kulenga lango baada ya penalti yake kwenda nje kufuatia madhambi ya Paul Ngalema dhidi ya Fred Lewis dakika ya 30.
Redondo alifunga bao la mapema zaidi mzunguko wa pili, baada ya kutumia dakika mbili tangu kuanza mpira kutikisa kamba za Lyon akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa.
Lyon walijibu shambulizi dakika ya nne na ustadi wa Juma Kaseja ulimnyima bao Jacob Massawe baada ya shuti lake kuchezwa na kipa huyo namba moja Msimbazi.
Mashuti mawili ya Ngassa dakika ya 4 na 6 yangeweza kubadilisha matokeo kama siyo kukosa shabaha na kwenda moja kwa moja mikononi mwa kipa wa Lyon, Abdul Seif.
Ngassa alirekebisha makosa yake kwa kufanya matokeo kuwa 2-0 baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Lyon akimalizia pasi ya Jonas Mkude.
Alikuwa Ngassa tena akipachika bao la tatu, la pili kwake kwenye mchezo huo shuti akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Haruna Chanongo dakika ya 35. Kipindi cha pili, Kocha Patrick Liewig aliwapumzisha Paul Ngalema na Mussa Mudde na kuingia Kigi Makasi na Komalibil Keita.

Mlinda mlango wa Afrikan Lyon akiondosha hatari langoni mwake.

Lyon walipunguza makali ya tofauti ya mabao ya kufungwa baada ya Bright Ike kumtungua Kaseja dakika ya 60 likiwa bao pekee kwao kwenye mchezo huo.
Pamoja na ushindi huo, Kocha Liewig alisema mchezo ulikuwa mgumu, ingawa pia hakusita kueleza hisia akiwalaumu wachezaji wake kucheza ovyo kipindi cha pili.
Mkwakwani Tanga, Union walifikisha pointi 25 na kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo kwa mabao ya Philipo Mutasela, Danny Lihanga na Haroun Mahundi, huku bao la Mgambo likifungwa na Peter Mwaliyanzi.




Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Tegete baada ya kutupia goli dhidi ya Prisons ambapo Yanga ilishinda 3-1.


Mabeki wa Prisons wakiondosha hatari langoni mwao

 

LIVERPOOL TOTTENHAM ZAFUNGASHIWA VIRAGO KOMBE LA FA

Tottenham imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la FA baada ya kulazwa magoli mawili kwa moja na Leeds United.

Luke Varney aliifungia Leeds bao lake la kwanza kabla ya Ross McCormack, kufunga la pili. Tottenham ambayo inashiriki katika ligi kuu ya Premier nayo ikapata bao lake kupitia kwa mchezaji wake Clint Dempsey.
 



Mtukutu El-Hadji Dioff akishangilia kuibandua Tottenham

Katika mechi nyingine Chelsea, nusura iage mashindano hayo baada ya kulemewa na Bendford.

Hata hivyo Fernando Torres aliifungia Chelsea bao lake la pili na kuiepushia aibu kubwa.

Timu hizo mbili zilitoka sare ya kufungana mabgoli mawili kwa mawili.

Liverpool vile vile, imeondolewa kwenye michuano hiyo ya FA, baada ya kunyukwa magoli 3-2 na Oldham, ambayo inashiriki katika ligi daraja ya kwanza.

Timu zingine za ligi kuu ambazo zimefuzu kwa raundi ijayo ni pamoja na Manchester United, Everton, Arsenal, Wigan, reading na Manchester City.

Norwich, QPR na stoke city zinaungana na timu ambazo zimefunganya virago vyao katika michuano hiyo ya FA.

Wachezaji wa Liverpool hoi baada ya kubanduliwa nje ya kombe la FA na Oldham

Wayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa


Wachezaji wa Oldham wakishangilia baada ya kuidungua Liverpool

Leeds 2-1 Tottenham
 
 
 
Oldham 3-2 Liverpool
Chelsea 2-2 Brandford

CLUB YA USIKU YA KISS YATEKETEA KWA MOTO WATU 233 WAFARIKI DUNIA

Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.

Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .

Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.


Baadhi ya ndugu ya waliopoteza maisha wakilia kwa uchungu

Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano

Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.

Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.

Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.

Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.

Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

Watu wakitimua mbio wakati moto ukiendelea kuwaka ukumbini hapo






Vikosi vya zima moto vikijaribu kuzima moto katika club ya disco ya Santa Maria