Monday, December 24, 2012

WISHING YOU A MERRY XMAS and A HAPPY NEW YEAR

CHELSEA YAIRARUA ASTON VILLA 8-0 HUKU SWANSEA WAKIIKALIA KOONI MAN UNITED

Chelsea imeiangushia kipigo kizito Aston Villa kwa kuicharaza magoli 8-0 katika mechi ya ligi kuu ya England, iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge, Jumapili.

Fernando Torres, ndiye aliyeanza kufungua karamu ya magoli kwa vijana wa Rafael Benitez, pale alipopachika bao katika dakika ya tatu ya mchezo.
David Luiz kiungo mahiri aliongeza goli la pili katika dakika ya 29 huku Branislav Ivanovic akishindilia goli la tatu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Ivanovic akitupia kwa kichwa goli la pili


Frank Lampard alifungua kipindi cha pili kwa bao lake la dakika ya 58 huku Ramires akifunga magoli mawili, na mengine yakifungwa na Oscar, Eden na Hazard wakifunga kila mmoja goli moja moja.

Ushindi huo umezidi kuiimarisha Chelsea katika nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England ikiwa na pointi 32 katika mechi 17 ilizocheza.
Katika mchezo mwingine uliochezwa Jumapili, vinara wa ligi hiyo Manchester United walitoka sare ya bao 1-1 na Swansea.

Patrice Evra aliifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 16 kwa njia ya kichwa kufuatia kona iliyochongwa na Robin van Persie.

Hata hivyo Michu aliisawazishia Swansea katika dakika ya 29.

Mpaka sasa Manchester United inaongoza ligi kuu ya England ikiwa na pointi 43 katika michezo 18, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 39 na Arsenal imejikita katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 30.

Michu akiisawazishia Swansea

Wayne Rooney akikukuruka


Michu akishangilia goli

Patrice Evra akishangilia goli
CHELSEA 8-0 ASTON VILLA

SWANSEA 1-1 MAN UNITED