Friday, December 14, 2012

KOCHA WA PSG YA UFARANSA KUMRITHI MILOVAN SIMBA S.C

Mabingwa wa Soka Tanzania,Bara Simba S.C  imemtangaza Patrick Liewig ambaye ni raia wa Ufaransa kuwa kocha mpya baada ya kusitisha mkataba na kocha wa sasa Mserbia Milovan Cirkovic. Liewig ameshazifundisha PSG ya Ufaransa, Club African ya Tunisia pamoja moja klabu kubwa barani Afrika ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Anatarajiwa kutua nchini baada ya wiki 2 kuanza kukinoa kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi.

Wasifu wa Lewig
Date of birth:04.10.1950
Age:62
Nationality:-France
ΓΈ-Incumbency as manager:1,97 Years
success-ratio as manager:30,77 % Wins
38,46 % Draw
30,77 % Loss
Preferred formation:4-2-3-1
 



Patrick Liewig

WIMBO WA LEO-Hatuna Habari nao (Abdu Kiba)


KASEJA APATA MRITHI KUTOKA UGANDA

Mabingwa wa Soka Bara, Simba wamekamilisha usajili wa mrithi wa kipa Juma Kaseja, Mganda Abbel Dhaira.

Dhaira amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola 40,000 (Sh43 milioni) na mshahara wa mwezi Sh2 milioni mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.

Kusajiliwa kwa kipa huyo kunakuja baada ya muda mrefu mashabiki wa Simba kuhoji kiwango cha Kipa Juma Kaseja.
Kaseja alikuwa gumzo kwa mashabiki wa Simba katika mechi za mwisho za duru la kwanza Ligi Kuu akituhumiwa kufungwa mabao ya kizembe.
Akizungumza jana baada ya kukamilika kwa usajili wa Dhaira, Hanspope alisema wanajivunia kupata kipa mwenye umbo kubwa kama Mohamed Mwameja aliyewahi kuidakia klabu hiyo.

Hanspope alisema kusajiliwa kwa kipa huyo Mganda kulitokana na mapendekezo kutoka kwa kipa wao wa kwanza hivi sasa, Kaseja.
“Kaseja ndiye aliyependekeza kwa uongozi kumsajili kipa huyu. Tunaamini mawazo yake yataisaidia Simba kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Dhaira alisema amefurahi kusajili Simba akiamini ni moja ya timu kubwa Afrika.
“Nimekuwa nikiisikia Smba kwa muda mrefu, nafahamu ni moja ya timu nzuri Ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla,” alisema kipa huyo.



Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba S.C Zakaria Hanspope akimkaribisha Abbel Dhaira


Golikipa kutoka Uganda Abbel Dhaira akiangusha saini na Dole gumba kuichezea Simba S.C kwa nyundo mbili



Abbel Dhaira akifanya vitu vyake uwanjani