Thursday, November 22, 2012

BENITEZ AVAA VIATU VYA DE MATTEO





Rafael Benitez kocha mpya wa Chelsea akitokea Liverpool na sasa amerithi mikoba ya De Matteo kuinoa Chelsea.


Roberto De Matteo kocha aliepigwa chini

ARSENAL YAUA MTU LIGI YA MABINGWA ULAYA



 






Jack Wilshere akimtoka mlinda mlango wa Montpellier na kutia kambani goli la kwanza kwa Arsenal katika dakika ya 49.


Podolski akitupia bao la pili na la ushindi la Arsenal dhidi ya Montpellier katika dakika ya 63

Katika mtanange huo uliohudhuriwa na watazamaji 59,760 Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo

Arsenal

  • 01 Szczesny
  • 03 Sagna
  • 04 Mertesacker
  • 05 Vermaelen
  • 06 Koscielny Booked
  • 08 Arteta
  • 10 Wilshere
  • 15 Oxlade-Chamberlain (Ramsey - 69' )
  • 19 Cazorla Booked (Coquelin - 84' )
  • 09 Podolski
  • 12 Giroud Booked (Gervinho - 84' )

Substitutes

  • 24 Mannone
  • 25 Jenkinson
  • 28 Gibbs
  • 16 Ramsey
  • 22 Coquelin
  • 23 Arshavin
  • 27 Gervinho

Montpellier

  • 16 Geoffrey Jourdren
  • 03 Mapou Yanga M'Biwa
  • 05 Bedimo Booked
  • 12 Congre
  • 21 El Kaoutari
  • 25 Deplagne Booked
  • 10 Belhanda
  • 13 Estrada (Joris Marveaux - 79' )
  • 20 Remy Cabella (Emanuel Herrera - 68' )
  • 08 Mounier
  • 09 Charbonnier (Martin - 68' )

Substitutes

  • 01 Laurent Pionnier
  • 04 Hilton
  • 27 Jeunechamp
  • 06 Joris Marveaux
  • 14 Pitau
  • 28 Martin
  • 11 Emanuel Herrera

MAN CITY YATOLEWA KIUME YATOA SARE NA REAL MADRID


Mfungaji wa goli la Real Madrid Karem Benzema akishangilia kwa staili ya aina yake.


Kun Aguero mfungaji wa bao la kusawazisha la Man City kwa njia ya penalti


Benzema akitupia kambani bao la kuongoza dhidi ya Man City



DI MATTEO APIGWA CHINI CHELSEA

Roberto De Matteo
 
Roberto Di Matteo amefutwa kazi na klabu ya Chelsea, baada ya kuwa meneja kwa kipindi cha miezi minane.

Di Matteo aliiwezesha Chelsea kuwa mshindi wa klabu bingwa barani Ulaya, na vile vile kupata Kombe la FA msimu uliopita, na mwezi Juni, alitia saini mkataba wa miaka miwli.

Lakini kufuatia Chelsea kuzabwa magoli 3-0 na Juventus usiku wa Jumanne, inaelekea timu hiyo itakuwa na kibarua kigumu sana cha kufanikiwa kuendelea katika michuano ya klabu bingwa, na kwa hiyo wasimamizi wa klabu wameonelea ni vyema kumtimua kutoka Stamford Bridge.

Kulingana na taarifa katika mtandao wa Chelsea, "klabu kitatoa taarifa kamili hivi karibuni kuhusiana na meneja wa timu".

Roman Abramovich, tajiri anayemiliki klabu ya Chelsea, sasa atakuwa anamtafuta meneja wa tisa, tangu kumiliki klabu mwaka 2003, na kwa muda mrefu, inaaminika amekuwa akizitamani sana huduma za aliyekuwa meneja wa Barcelona ya Uhispania, Pep Guardiola.

Lakini vile vile amewasiliana na aliyekuwa kocha wa Liverpool ya Uingereza, Rafael Benitez, na kuna uwezekano huenda akashikilia hatamu kwa muda mfupi.

Abramovich, raia wa Urusi, tayari alikuwa amewasiliana na Benitez hata kabla ya Chelsea kushindwa nchini Italia.