Monday, September 24, 2012

MAN U YAITULIZA LIVERPOOL ARSENAL MAN CITY HAKUNA MBABE


Manchester United imeicharaza Liverpool kwa bakora 2-1 katika dimba la Anfield katika mpambano ulioshuhudiwa na mashabiki wapatao 44,263. Liverpool ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Man Unietd kupitia kwa Steven Gerrald katika dakika ya 45. Mpaka mapumziko bao lilikuwa 1-0 wenyeji akienda kupumzika kifua mbele.

Kipindi cha pili nibeebe nibeebe nibebeee ilianza na katika dakika ya 50 R Da Silva aliipatia Man U bao la kusawazisha kabla ya Robin Van Persie kutupia kambani goli la pili na la ushindi katika dakika ya 80 kwa nduki kali ya mkwaju wa penati.