Monday, August 27, 2012

WANAMUZIKI 10 MATAJIRI ZAIDI AFRIKA


1-Youssou Ndour

Youssou Ndou ndiye mwanamuziki tajiri zaidi barani Africa. Mshikaji anamiliki kituo kikubwa zaidi binafsi cha luninga nchini Senegal, kampuni ya magazeti na kituo cha radio.

Anamiliki pia Klabu ya Usiku(night club) na record label. Anamiliki kampuni ya nyumba na makazi. Mwaka 2004 jarida la Rolling Stone lilimwelezea kama mwanamuziki maarufu zaidi nchini Senegal na pengine barani Afrika aliye hai.
Tangu April 2012, ni waziri wa utalii na utamaduni nchini Senegal.

2-P Square
 
Hakuna msanii wa kizazi cha leo anaeweza kugusa matawi ya mapacha hawa, Peter na Paul Okoye. Wana hela chafu!
Wanachaji dola 250,000 kwa kila show ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 390 za Tanzania! Kuongezea msumari zaidi hapo ni kwamba hawa Washkaji wana show kila weekend! Mpaka sasa hivi wameshafanyiwa booking ya kufanya show sehemu mbalimbali duniani hadi March mwakani!
Nyumba yao waliyoipa jina la Squareville huko Ikeja Nigeria ina thamani ya dola milioni 3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 4.
Waliweka historia kwa kuwa wasanii wa kwanza kununua kiwanja kwenye eneo la Banana Island nchini Nigeria ambacho kina thamani ya zaidi ya dola milioni 3 pia!
Wana mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya pili kwa ukubwa ya simu nchini Nigeria ya Globacom wakiwa kama mabalozi wake ambapo hulipwa dola milioni 1 kwa mwaka, wanamiliki pia mijengo kibao ya kupangisha.Ucpime jipangeee!
 
 
3-D Banj
Mnigeria huyu aliye chini ya label ya Kanye West, G.O.O.D Music, alitengeneza takriban dola milioni 5 kwenye kampeni ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.
Anamiliki jina la ‘Koko’ linalojumuisha klabu bora za Nigeria za KokoLounge, maji ya kunywa Koko Water na Koko Mobile.
Aliwahi kufanya reality show ya TV iitwayo Koko Mansion na kulipwa dola milioni 1.Anamiliki nyumba yenye thamani ya dola milioni 1.5 jijini Atlanta. Ni mwenyekiti mtendaji wa Dbanj Records na pia ana kampuni ya ulinzi iliyofanikiwa sana.
Yeye hucharge dola 100,000 kwa show.



4-Koffi Charles Antony Olomide
Mfalme wa Lingala Koffi  anacharge tabriban Euro 100,000 kwa show. Jamaa hupiga show nchini Ufaransa zinazojaza karibu watu 80,000 ambapo tiketi moja ni Euro 30 sawa na shilingi elfu 60.Amekwishatoa albam zaidi ya saba ambazo zimemuingizia mamilioni ya dola.
 
5-Salif Keita
Salif Keita ukipenda unaweza kumuita  ‘Sauti ya dhahabu ya Africa’, ni miongoni mwa watu wanyenyekevu lakini matajiri sana barani Afrika.Msanii huyo albino anamiliki kisiwa chake binafsi nchini Mali.Anamiliki majumba na mali zingine nchini Ufaransa na Mali.

6-Fally Ipupa
Msanii huyu anajulikana kama ‘Mfalme mpya wa Lingala’ wa DRC. Kutoka kuwa mcheza show wa zamani wa Koffi Olomide, anasifika kwa kuleta usasa zaidi kwenye muziki wa Lingala. Ameshakuwa balozi wa brand nyingi za nguo nchini Ufaransa, concerts zenye gharama na kuuza kopi kibao za albam zake.
 
7-2 face idibia
Msanii huyu wa Nigeria anamiliki nyumba za kupangisha zenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.Hulipwa kuanzia dola 50,000 - 80,000 kwa show.namiliki pia klabu ya usiku ya nguvu na biashara zingine zinazomuingizia hela nyingi.
8-Hugh Masekela
Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa Jazz wanaoheshimika zaidi barani Africa. Anamiliki mobile studio yenye mafanikio makubwa nchini Botswana. Hushiriki kwenye matamasha makubwa duniani na huingiza mamilioni ya dola kutokana na mauzo ya albam zake.
9-Banky W
Ukiweza muite Mr. Capable pia. Banky W hufanya show mara tatu ama nne kwa wiki zinazomuingiza mshiko mrefu mno. Aliwahi kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Estisalat ya Nigeria ambapo alitumika kwenye matangazo yake.

Kwa sasa ni balozi wa Samsung Mobile. Amewahi kufanya kampeni ya Coca Cola-Nigeria na Microsoft’s Anti-cyber Crime Initiative.
Kutokana na kuingiza hela nyingi amenzisha mradi kuwasaidia wasiojiweza kwa kuwalipia ada watoto wenye uwezo darasani chini ya Mr. Capable Foundation.

10-Chameleone
Mzee wa Valuvalu anafunga list kwa kuwa msanii mwenye hela zaidi kuliko wote Afrika Mashariki.Anamiliki gari Cadillac Escalade yenye thamani kubwa, Mercedes Benz ML 320, Super Custom, convertible na Premio.

Anaishi kwenye nyumba yenye gharama kwenye maeneo ya wazito huko Seguku Hill kwenye viunga vya Kampala, simu zake mwenyewe na mali zingine nyingi.

Matumizi ya nyimbo zake yanamuingiza mamia kwa maelfu ya Euro!

DIAMOND AMSHIRIKISHA J MARTINS KWENYE SONG JIPYA


Naseeb Abdul "DIAMOND"

J Martins

Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu kwenye shoo ya Big Brother Africa nchini Afrika ya Kusini, Diamond alianza kupata mialiko mbalimbali kutoka kwa wasanii wakubwa barani Afrika, na hivi sasa anatarajia kukamilisha kolabo yake anayoifanya na mwanamuziki kutoka Nigeria J Martin.

Kwa mujibu wa Diamond hivi sasa amesharekodi sehemu zake kwenye wimbo huo katika studio za MJ Records chini ya Prodyuza Marko Chali.

"Ingawaje nipo katika mchakato wa kusafiri kuelekea Marekani, lakini tayari nimeshaingiza voko za kazi yangu kwa Marco Chali na punde kolabo hiyo itaiva kama ilivyopikwa katika chungu safi.

"Chorus ya wimbo huo nimeimba mimi na mcheza shoo wangu Mose Iyobo"
anasema Diamond ambaye ameamua kumpa shavu dansa wake kutokana na kuonyesha uwezo mzuri katika kuimba.

J Martin ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akichukua kozi maalum ya miezi mitatu ya masuala ya utayarishaji, tayari anausubiri wimbo huo ili aingize sauti yake.

Katika safari hii Diamond anakwenda na madansa wake wote wanne na msemaji wake. Diamond atafanya shoo katika mkutano mkubwa unaofanyika Marekani ambao wahudhuriaji wamemtaka akawape burudani.

WAZIRI WA USALAMA LIBYA AJIUZULU


Waziri wa usalama wa Libya aliejiuzulu Fawzi Abdel A'al

Taarifa kutoka Libya zinasema kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Fawzi Abdel A'al, amejiuzulu.
Sababu ya kujiuzulu kwake haijafahamika mara moja.

Kujiuzulu kwa bwana Fawzi kumetokea siku moja baada ya polisi katika mji mkuu, Tripoli, kutuhumiwa kushindwa kuwazuwia Waislamu wenye msimamo mkali wasibomoe msikiti na kaburi la Wasufi mchana kweupee.