Tuesday, August 21, 2012

EVERTON YAIDUNGA MAN UNITED KIMOKO


Fellaini akipiga kichwa kilichozama moja kwa moja kambani kuandika goli la pekee la Everton

Kimuhemuhe cha ligi kuu ya Uingereza kimendelea jana jumatatu huku mamilioni ya mashabiki wa soka duniani wakishuhudia Timu ya Everton ikichabanga Manchester united kwa bakora moja kwa yai katika dimba la Goodison Park, mchezo huo ulishuhudiwa na watazamaji wapatao 38,415.

Katika mtanange huo goli la pekee la Everton lilitupiwa kambani na Fellaini katika dakika ya 56 na kuwaacha hoi Man United.


Cleverley wa Man U akioneshana umwamba na Pienaar wa Everton

Fellaini akishangilia goli

Hapa kazi tuu..Welbeck akiwa chini ya ulinzi mkali


Van Persie akitia mchomo katika mpambano huo

Ngoma ngumu..Rooney na Kagawa wakiwa wameloa baada ya kuchapwa goli la kwanza
 


Daah hivi kweli tumechapwa?

UNAONA UTAAAAAAAMU MAMBO YA BAIKOKO

WAZIRI MKUU ETHIOPIA AAGA DUNIA

Aliekuwa waziri mkuu wa Ethiopia marehemu Meles Zenawi

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka hamsini na saba na ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala wake ulikumbwa na utata barani afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga ameiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.
Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua wadhifa huo.