Thursday, August 16, 2012

KOFFI OLOMIDE AMPA KISAGO PRODUCER, AFIKISHWA KWA "PILATO"

Koffi Olomide performing in 2005
Koffi Olomide akipiga show kabla ya kudakwa na wama usalama
 
Mwanamuziki mashuhuri wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo(DRC) Koffi Charles Antony Olomide amewekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kumshambulia mtayarishaji wake wa muziki(Producer).
 
Koffi alitiwa mikononi mwa polisi siku ya jumatano baada ya "Fracas" katika Hotel moja ilioyopo katika mji mkuu wa DRC Kinshansa, Umati wa watu ulifurika katika chumba mahakama kumuona mwanamuziki huyo akipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia Producer wake. Katika kesi hiyo Koffi Olomide anatetewa na mawakili 10.
 
Habari zaidi zinasema Koffi Olomide anamdai Producer huyo kiasi cha Euro 3,000 sawa na dola za kimarekani  3,680 na ni sawa na Paundi za Uingereza 2,345 na ni zaidi ya Shilingi za Kitanzania 5,800,000.
 
Mwanamuziki huyo anaepiga muziki wa dansi kwa staili ya SOUKOUSS neno linalotokana na neno la kifaransa "Secouer" Likimaanisha "Tingisha", Kesi yake iliahirishwa na kama akipatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela
 
 
 

SONG: KIGOMA ALL STARS-Leka DUTIGITE!

CHADEMA KUZINDUA TAWI HOUSTON MAREKANI Agosti 25,2012


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewatangazia wananchi wote kuwa Siku ya Jumamosi Aug 25 kutakuwa na ufunguzi rasmi wa tawi la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jijini Houston, Texas Nchini Marekani
Wageni rasmi wa ufunguzi wa tawi hilo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Jodeph Mbilinyi a.k.a Mr II/Sugu
Sherehe za ufunguzi wa tawi hilo zitaanza mida ya saa 5:PM (Jioni).

MASIKINI FABRICE MUAMBA, MPIRA NDIO BASI TENA


Fabrice Muamba

Mchezaji mahiri wa Timu ya Bolton Wanderers inayoshiriki ligi kuu ya Barclays Nchini Uingereza Fabrice muamba amestaafu rasmi soka baada ya kupokea ushauri wa mwisho kutoka kwa jopo la madaktari bingwa wa moyo na klabu ya Bolton ilitangaza rasmi Muamba kutocheza tena soka kufuatia matatizo ya kiafya.

Muamba akiongea kwa huzuni alisema amekuwa na ndoto za kurudi uwanjani na kukipiga katika klabu yake ya Bolton siku zote alizokuwa katika matibabu.
"Tangu kipindi nilipopata mshtuko wa moyo na kutolewa hospitalini, Nilikuwa na matumaini makubwa ya kuendelea na mchezo wangu wa soka na kuichezea Bolton Wonderers kwa mara nyingine" Alisema Muamba kwa huzuni kubwa.

Wiki iliyopita Muamba alisafiri mpaka Ubelgiji kwenda kufanyiwa oparesheni ndogo ya moyo na madaktari kumshauri kwasasa asahau kukipiga kutokana na hali ya afya yake.
Haya ndio maneno ya Fabrice Muamba wakati akitangaza kustaafu soka kutokana na matatizo ya kiafya.

“I have remained utterly positive in the belief I could one day resume my playing career.

“But the news was obviously not what I had hoped it would be and I am now announcing my retirement.
“Football has been my life. I count myself very lucky to have been able to play at the highest level.
“While the news is devastating, I have much to be thankful for.
“I thank God that I am alive and I pay tribute once again to the members of the medical team who never gave up on me.
“I would also like to thank everyone who has supported me throughout my career, and the Bolton fans.
“I am blessed to have the support of my family and friends at this time.”


Soma zaidi hapa: http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/4488759/Fabrice-Muamba-retires-Bolton-ace-quits-over-heart-fears.html#ixzz23gqM1Uop Ikumbukwe Muamba al manusra apoteze maisha baada ya kuzimia kwa dakika 78 alipozirai wakati wa mechi kombe la FA kati ya Bolton na Tottenham katika dimba la White Hart Lane Machi 17,2012. Nae Mchumba wa Muamba, Shauna Muamba alikuwa na haya ya kusema “Thanks for all the support. We’re blessed to have our family and we’re looking forward to whatever the future holds.”
Soma zaidi hapa: http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/4488759/Fabrice-Muamba-retires-Bolton-ace-quits-over-heart-fears.html#ixzz23grXAMIL



Daaah jembeee, pole sana yote maisha cha muhimu ni kumshukuru mungu kuwa upo hai mpaka leo baada ya kuzimia kwa masaa 78.

Picha za siku Muamba alipozima ghafla uwanjani







Fabrice Muamba katika uzi wa Bolton kabla ya kupatwa na matatizo ya kiafya(moyo).

STARS NGUVU SAWA NA BOTSWANA


Erasto Nyoni mfungaji wa goli la kwanza la Stars katika mazoezi kabla ya kuivaa Botswana

Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa leo (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.

Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa naLemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.

Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd. Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.

“Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
“Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza. Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole,” alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.

Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi,
Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani kesho (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
(Afisa habari TFF)

MGHANA WA SIMBA KUIKOSA LIGI KUU, YAWANIA JEMBE LINGINE KUTOKA MALI

KLABU ya Simba imesema mchezaji Aboul Karimu kutoka Mali atafanya majaribio na klabu hiyo hivi karibu na kama atafanya vyema hivyo atapewa nafasi ya kuitumikia klabu hiyo ya msimbazi.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema Simba imekuwa na mazungumzo na wakala wa kimataifa Valer St.Clair kuhusu majaribio ya mchezaji huyo raia wa Mali.

“Endapo atafanikiwa kwenye majaribio anaweza kuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa kwenye dirisha la usajili na hivyo kupata nafasi ya kuitumikia timu ya Simba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara na ligi Mabingwa Afrika,” alisema Kamwaga.
Mchezaji huyo anatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa wiki hii na kuanza majaribio wakati dirisha la usajili likiwa linafikia tamati Septemba 10.

Vile vile klabu ya Simba jana ilichukua fursa ya kuwatambulisha wachezaji wake wapya wa kimataifa, MKenya Pascal Ochieng na Mghana Daniel Akuffor.

Kamwaga alisema beki wa kati Pascal Ochieng atachukua majukumu hayo kwenye Ligi Kuu ambayo iko karibuni kuanza wakati Daniel Akuffor atakuwa akiichezea wekundu wa msimbazi kwenye ligi ya mabingwa ya Afrika.

Kamwaga pia alisema Simba imeweka wazi kwamba mkataba wa Mchezaji mpya Daniel Akuffor utamalizika Mei mwakani.

Alisema,“mkataba wetu na Akuffor mwisho mwezi wa tano na hivyo kwenye makubaliano yetu hatacheza Ligi Kuu ila ataiwakilisha Simba kwenye ligi ya mabingwa ya Afrika.”

Simba itashiriki kwenye ligi ya mabingwa Afrika itakayoanza mwaka huu baada ya kutwaa kombe la ligi kuu ya Tanzania bara wakati huo huo timu ya Azam iliyomaliza katika nafasi ya pili itashiriki kwenye kombe la Shirikisho Afrika.