Tuesday, June 26, 2012

STAR WA BONGO MOVIE FLORA MVUNGI KATIKA KASHFA YA UTAPELI WA 200,000/=


Flora Mvungi

Star maarufu katika tasnia ya filamu za kibongo "Bongo Movies" Flora Mvungi ameshutumiwa kupokea mlungula wa kiasi kadhaa unaofikia shilingi za kibongo laki mbili (200,000) kutoka kwa mtayarishaji wa filamu chipukizi aliejulikana kwa jina moja la Othman.

Akielezea mkasa huo wa "kupigwa" Tshs 200,000/= za kibongo na staa wa filamu nchini Mtayarishaji huyo wa filamu a.k.a Producer amesema Alikubaliana na Flora ampatie kiasi hicho ili aweze kushiriki katika filamu anayoiandaa inayoenda kwa jina la MZIWANDA. Othman anasema walipokubaliana alimtumia Flora mkwanja huo kwa njia ya Tigopesa, lakini ilipofika muda wa kuwa mahala pa kutayarisha filamu (Location) Staa huyo hakutokea kwa visingizio lukuki. Lakini Producer huyo akafunguka kuwa safari hii ilikuwa mara ya nne kuzinguliwa na Flora katika maswala mazima ya kufika eneo la tukio maarufu kama Location.

Producer Othman alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja maarufu cha redio hapa nchini alifunguka hayo na ndipo mtangazaji wa kipindi hicho alipoamua kuwaunganisha kwa njia ya simu, katika hali ya mshangao staa huyo alikana kumfahamu Producer huyo wa movie za kibongo lakini alikiri kuwa kuna filamu ambayo aliitwa akashiriki lakini kutokana na sababu fulanifulani hakufika na akaahidi aitwe mambo yatakapokuwa tayari.
Utamu ukanoga pale mtangazaji alipomvutia kamba Flora Mvungi na kisha akamuuliza maswali kadhaa halafu akamuweka hewani wapeane makavu na producer, Hali ilikuwa ya majibizano makali Flora akikana kupokea mkwanja hali iliyoonekana kumkera zaidi Producer huyo na akisisitiza kuwa staa huyo asijifanye mjanja kwani yeye ana uthibitisho wa Message alizomtumia pesa ghafla Flora akakata simu nganjaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! Hali hii iliacha SINTOFAHAMU ikiwa imetanda katika sakata hilo.

DOGO JANJA AFANYA KUFURU MLIMANI CITY, MANUNUZI MIL 2.5


Abdul Aboubakar Chande "Dogo Janja"

Unaweza usiamini na huenda ukahisi labda ni story za town, lakini ukweli ndio huo, Siku chache baada ya kutua Bongo na Pipa (Ndege) akitokea Kilimanjaro na kujiunga na kampuni ya Mtanashati Entertainments ya jijini, nyota wa Bongo Fleva , Abdul Abubakar Chande ‘Dogo Janja’ mwishoni mwa wiki iliyopita alisomea kisomo maalumu cha kuomba Mwenyezi Mungu amnyooshee mambo yake na "umatemate" zaidi pindi atakapoanza kushusha ngoma mpya.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kisomo hicho kichoshudiwa na Teentz.com, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ostaz Juma na Musoma alisema kuwa wameamua kumfanyia kisomo hicho kwa lengo la kuweka kazi zote za Dogo janja mikononi mwa Mungu kwa kuwa wanaamini wapo watu ambao hawajafurahishwa na mpango mzima wa dogo huyo kurejea Bongo

Katika shopingi hiyo Dogo janja alitumia zaidi ya shilingi Milioni 2.5 za kibongo kununua vitu mbalimbali, kama Seti 5 za viatu, Suti 4, Jeans 10, T shirt 10,miwani 5, simu aina ya BlackBerry, Laptop na vitu vingine kibao .
Huku akionekana mwenye furaha kubwa Dogo Janja aliiambia Teentz.com kuwa amefuahi kwa kiasi kikubwa kwa yale yote ambayo Ostaz Juma na kundi zima la Mtanashati kwa yote wanayomfanyia hivi sasa kwani hatakuwa na malipo mengine zaidi ya kuwafanyia kazi nzuri zenye kiwango.

“Nina furaha sana, hakika namshukuru Ostaz kwa yote anayofanya kwangu sina la kusema zaidi wasubiri ngoma za kweli zitakazokuwa kama shukurani kwao kwa sababu ndiyo kitu pekee ambacho naweza kukifanya kwao” alisema Dogo Janja.


VENUS WILLIAM AONDOLEWA MAPEMA WIMBLEDON


Venus akirudisha mchomo kwa mpinzani wake Elena Vesnina

Bingwa mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus Williams, amesema hana nia ya kuachana na mchezo huo baada ya kuondolewa katika siku ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza, alipopokea kipigo kitakatifu kutoka kwa mchezaji Mrusi, Elena Vesnina.
Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome, alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu.
Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni.

Kiboko ya Venus Williams,Elena Vesnina akipeleka mchomo kwa Venus

"Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alielezea Williams.

"Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu."

Mara ya kwanza Williams kushindwa katika raundi ya kwanza ilitokea mwaka 1997, wakati alipoingia pambano lake la kwanza la Wimbledon, na wakati huo alikuwa hata hayumo miongoni mwa wale waliopangwa katika mashindano hayo kama wachezaji bora.

Ni wanawake wawili tu ulimwenguni ambao wameshawahi kupata ubingwa wa Wimbledon mara nyingi kumshinda Williams, lakini tangu mwaka 2008, hajawahi kuibuka bingwa wa mashindano hayo.

Mara tu baada ya ushindi wake wa mwisho, iligunduliwa kwamba anaugua ugonjwa wa Sjogren's Syndrome, na ambao humfanya mgonjwa kujihisi ni mchovu mno, na katika sehemu mifupa inaungana, maumivu.

Ayaaaaaaaa nimechapwa!!!!!


Kudadekii leo Venus hutoki hapa!!

Venus Williams baada ya kupokea kichapo kitakatifu kutoka kwa Mrusi Elena Vesnina