Monday, June 25, 2012

EURO 2012 ITALIA YATINGA NUSU FAINALI WAKATI ASHLEY WAWILI WAKIIGHARIMU UINGEREZA


Barwuah Balotelli akipiga tik-tak ambayo ilipaa langoni mwa Uingereza

Gianluigi Buffon akiokoa mchomo wa Johnson ambao almanusra uzae bao kwa Uingereza

Timu ya soka ya Uingereza imetupwa nje katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kunyukwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa changamoto ya mukwaju ya penalti 4-2 mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.

Italia sasa itavaana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.
Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.

Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda Italia.

Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.

Kadri mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio za kutegemewa tena.

Baada ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: "Wachezaji walicheza kadri ya uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti, lakini mambo hayakuwa hivyo. Ukiongoza katika penalti, unashikilia matumaini kwamba mambo yatasalia hivyo, lakini Italia ndio waliokuwa na bahati. Vijana waliokuwa walinzi walifanya kazi nzuri mno, na kuiletea nchi fahari, lakini tunarudi nyumbani na mioyo ya huzuni, na hili ni jambo gumu kulikubali."

England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
Balotelli akijaribu kombora langozi mwa Uingereza bila matumaini
England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
Ngoma inogile Lescott na Balotelli
England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final

England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final

England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
Imooooo..Joe Hart akichumpa kuokoa penati bila mafanikio
England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
Wachezaji wa Uingereza waliokosa penati A.Cole na A.Young na wenzao wakiwa hawaamini kilichojiri katika dimba la Olympic mjini Kiev

England v Italy - UEFA EURO 2012 Quarter Final
John Terry akimtuliza Ashley Cole na Jermain Defoe akimtuliza Ashley Young baada ya Ashley wawili kukosa mikwaju ya penati katika mtanange dhidi ya Italia

Mikwaju ya penati Uingereza na Italia