Friday, June 22, 2012

CHRISTIANO RONALDO AIPELEKA URENO NUSU FAINALI EURO 2012


Gooooooooo!! Christiano Ronaldo akitupia kambani kwa kichwa maridadi

Woyoooooo nimemaliza kaziiiiiii!!! Ronaldo akishangilia goli lililoipeleka Ureno nusu fainali

Mshambuliaji hodari Christiano Ronaldo aliwaridhisha mashabiki wa Ureno kwa kucheza vizuri sana usiku wa Alhamisi, na juhudi zake zimeiwezesha Ureno kuifumua Jamhuri ya Czech bao 1-0 na kufanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Ronaldo, ambaye alifunga magoli mawili wakati Ureno ilipocheza na Uholanzi, aliweza kuichachafya ngome ya Czeck na mashuti mawili kugonga mlingoti wa goli.

Hatimaye aliweza kutupia kambani kwa kichwa, huku zikiwa zimesalia dakika 12 kabla ya mechi kumalizika, na kipa Petr Cech akiweza kuufikia mpira, lakini hakuweza kuuzuia kutokana na nguvu nyingi zilizotumiwa na Ronaldo.


Peter Cech akikabiliana na Christiano Ronaldo

Ilikuwa dhahiri kwamba wachezaji wa Czech waliingia uwanjani wakiwa na nia ya kuimarisha ngome yao, na wala sio kushambulia, na kamwe hawakumtisha kabisa kipa wa Ureno.

Ureno sasa itakutana aidha na Uhispania au Ufaransa katika juhudi za kufuzu kwa fainali.

Bila shaka timu ambayo itakutana na Ureno itakuwa na wasiwasi ni vipi itaweza kumzuia Ronaldo, ambaye baadhi ya wadau wa soka wanasema kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi barani Ulaya.

Kiungo Miguel Veloso akimrukia Ronaldo kwa furaha

Portuguese Football Fans AFP/Getty Images
Mashabiki wa Soka wa Ureno wakiwa katika viwanja vya Campo Pequeno Square jijini Lisbon,Ureno wakiangalia mechi ya nusu fainali kati ya chama lao na Jamhuri ya Czech mechi iliyokuwa ikipigwa katika dimba la Warsaw nchini Poland. 

PORTUGAL  1-0  CZECH REPUBLIC