Tuesday, May 29, 2012

PETER CECH AONGEZA 'NYUNDO' NNE CHELSEA

Petr Cech - Chelsea v Sunderland - Premier League
Petr Cech - Chelsea v Sunderland - Premier League
Petr Cech - Chelsea Training Session
Golikipa Peter Cech

Petr Cech ameamua atasalia katika klabu ya Chelsea, angalau kwa miaka mine ijayo, kufuatia kutia saini mkataba wa muda huo.
Kipa huyo ambaye amehudumu Chelsea kwa muda mrefu, ameichezea timu ya The Blues katika mechi 369, tangu alipojiunga na klabu mwaka 2004.
Petr Cech
Peter Cech ataichezea Chelsea kwa miaka minne zaidi
Sasa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016. "Ninafurahi mno kuwa ni sehemu ya klabu hii maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
"Ninatumaini miaka hiyo minne ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea klabu."
Cech, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
Baadhi ya mafanikio ya Chelsea Cech akiwa ni kipa ni pamoja na kupata ubingwa wa ligi kuu ya Premier mara tatu, ubingwa wa Kombe la FA mara nne, ushindi wa Kombe la Carling mara mbili, na hivi majuzi, ubingwa wa UEFA wa klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.
Cech pia alitangazwa kama mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
"Chelsea inatambua kikamilifu mchango muhimu kutoka kwa Petr wakati huu wa klabu kupata ufanisi wake mkubwa zaidi katika historia yake," alielezea mkurugenzi mkuu wa Chelsea, Ron Gourlay.
Kipa msaidizi wa Cech, Thibaut Courtois kutoka Ubelgiji, huenda akaachiwa mechi zaidi za ligi kuu ya Premier ili kujinoa zaidi, baada ya kuonyesha uhodari wake akiwa mchezaji wa mkopo katika klabu ya Uhispania ya Atletico Madrid, ijapokuwa kijana huyo wa miaka 20 huenda akaazimwa kwa timu nyingine kwa muda mfupi.
Courtois alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Racing Genk, mwezi Julai mwaka jana, na kwa kuelekea Uhispania na kutofungwa, aliiwezesha klabu ya Atletico Madrid kuibuka mabingwa wa klabu ya Europa mapema mwezi huu.
Peter Cech akifanya vitu vyake

PICHA YA SIKU (PHOTO OF THE DAY)