Friday, May 25, 2012

MODEL OF THE DAY





RATIBA YA MSAFARA KUELEKEA DAR-LIVE KATIKA SHEREHE ZA KUIPONGEZA SIMBA SPORTS CLUB KWA KUTWAA UBINGWA

DROGBA ASEMA CHELSEA SASA BHAAAAS..NASEPA!


Didier Drogba

Mshambuliaji Didier Drogba ataihama timu ya Chelsea ya England msimu huu wa joto, baada ya kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka 8.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na mwenye umri wa miaka 34, alitia kambani bao safi na la ushindi katika fainali ya mwaka huu ya Kombe la klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern.

Drogba atakuwa huru kujiunga na klabu yeyote ile, kwani mkataba wake na timu ya Chelsea The Blues unaelekea kumalizika.


Drogba akiwa na kombe la ligi ya mabingwa Ulaya walilolitwaa mwaka huu mbele ya Bayern Munich huko Ujerumani.

Baada ya miezi mingi ya mashabiki kutojua hatma yake, Drogba amethibitisha sasa ataondoka Stamford Bridge.

"Nilitaka kukomesha hali hii ya shaka na kuthibitisha kwamba ninaondoka Chelsea", alielezea Drogba katika tovuti ya Chelsea.

"Umekuwa ni uamuzi mgumu sana kwangu, lakini ni fahari kwangu kwa ufanisi tulioweza kupata, lakini wakati umewadia kwa changamoto mpya", alielezea.

Aliongezea: "Kama timu, tumefanikiwa katika mengi, na tukishinda vikombe muhimu."

"Ningelipenda kuitumia nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu, hasa Roman Abramovich na wachezaji wenzangu."



Tatizo la mkataba wa Drogba ulianza msimu uliopita, wakati klabu ilipokataa kumuongezea miaka miwili zaidi katika mkataba wake.

Wasiwasi wa mashabiki ulizidi wiki chache zilizopita, iwapo Drogba ataendelea kuichezea Chelsea, hasa baada ya timu yake kuibuka mshindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool, na pia alipofunga bao la kusawazisha Jumamosi, na vilevile kufunga goli la ushindi wakati wa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Bayern.

NCHUNGA AACHIA KITI KUINUSURU YANGA..Chezea wazeiya weye!!!


Mwenyekiti wa Yanga alieachia ngazi Lloyd Nchunga

Vicky Kimaro(Gazeti la Mwananchi)SIKU moja baada ya kuvamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kundi la watu wasiojulikana Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga amejiuzulu kuiongoza klabu hiyo.

Nchunga alitangaza uamuzi huo wa kujiuzulu jana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi yake iliyopo jengo la NSSF Akiba mbele ya waandishi wa habari wachache.

Alisema,"sipo tayari kuona klabu Yanga inahujumiwa kwa vile tu mimi ni kiongozi, Kamati ya Utendaji na wale walioteuliwa chini ya ibara ya 29(3) ya katiba ya Yanga pamoja na bodi ya wadhamini, itawaongoza wanachama mpaka kufikia mkutano mkuu kwa mafaniko zaidi."

"Kwa hekima nimeamua kujiuzulu nafasi yangu katika Uenyekiti wa Yanga kwani ni klabu ninayoipenda hata kama mimi sio kiongozi kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba yetu,"alisema Nchunga.

Katika siku za hivi karibuni Nchunga amejikuta kwenye mgogoro mkubwa na Baraza la Wazee la klabu hiyo ambao walikuwa wakimshinikiza ajiuzulu kwa madai kuwa ameisababisha madeni makubwa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mwenendo mbovu wa timu yao huku wakidai wachezaji wamekosa nidhamu.

Pia wazee hao walikuwa wakimlaumu Nchunga kwa kusababisha Yanga kupata matokeo mabovu katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba walipofungwa mabao 5-0 katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania bara.

Nchunga akizungumza jana na waandishi wa habari alisema kitendo kinachofanywa na Baraza hilo la Wazee wakiongozwa na Ibrahimu Akilimali ni usaliti mkubwa ulioambatana na matukio mbalimbali yanayoendelea ndani ya klabu hiyo hadi kuupindua uongozi wake.

"Siwatuhumu wachezaji moja kwa moja, isipokuwa mfululizo wa matukio wiki tatu kabla ya mchezo na Simba inaonyesha kulikuwa na usaliti mkubwa ambao hatukuweza kuubaini mapema,"alisema Nchunga.

"Sioni mantiki kwa hoja kuwa tulifungwa kwa vile wachezaji walikuwa wakidai mishahara, posho, au eti mtendaji wetu alishikiliwa Arusha kwa deni la hoteli, ndiyo tuvune bao tano,"alisema Nchunga.

Alisema,"kwa wanaoijua Yanga wanafahamu Yanga imewahi kuwa na madeni makubwa katika hoteli mbalimbali, mawakala wa ndege na baadhi tumeyakuta sisi na kuyalipa, hii imewahi kutokea kabla na wakati akiwapo mfadhili, sembuse sisi tulioachwa baki na bado wachezaji walicheza kwa morali?."

"Uongozi wangu ndani ya mwaka mmoja tumechukua mataji matatu, ubingwa wa Ligi Kuu, 2011/2012, Kombe la Kagame na Ngao ya Hisani ukiachia mechi ya Mei 6 ambayo tulifungwa magoli matano,"alisema Nchunga.

Alisema,"tumefanikiwa kuboresha mkataba wetu na TBL, tumeingia mkataba na Nexus Ltd ambao inatutafutia wadhamini wa ndani na nje, tumefanya kampeni kupitia mitandao na kukusanya data za wanachama na kusajili wapya lengo likiwa ni kukusanya Sh3,000,000 hadi 8,000,000 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu."

Nchunga alisema,"hayo yote tulifanya ili kuondokana na utegemezi wa ufadhili wa mtu mmoja na tayari tulishatuma maombi kwa msajili Manispaa ya Ilala ya kuanzisha Saccoss ya Yanga."

"Utamaduni wa kutimuana baada ya matokeo mabaya ni dhambi ambayo itatutafuna kama hatutaiacha, kwani wenye hila na uchu wa madaraka wataendelea kutumia mbinu hiyo ili kuondoa uongozi wa kidemokrasia,"alisema Nchunga akiwa na sura ya huzuni.

Alisema,"baada ya Mapinduzi kushindikana na TFF kuonya, wazee wakiongozwa na Akilimali wamesikika katika kipindi cha michezo cha radio moja wakidai ni bora Yanga ishushwe daraja au kufungiwa kuliko mimi kuendelea kuongoza.

Katika hatua nyingine Nchunga pia, alisema jana majira ya saa nane usiku alisikia mbwa wakibweka kwa nguvu huku taa za alamu zikipiga kelele mfululizo kitendo ambacho kilimstua na alipochungulia dirishani aliona kundi la watu wanaokadiriwa kufikia 15 wakiwa kwenye harakati za kutaka kuingia ndani kwake.

"Baada ya kusikia kelele zile za alamu na mbwa tuliwapigia simu walinzi wetu wawili kumbe na wenyewe walikuwa wameshafanya jitihada za kutafuta nguvu kwa walinzi wengine kitendo kile kililiogopesha kundi lile na kukimbilia bondeni, hata hivyo tulipiga simu polisi ambao walifika na kukuta kundi hilo limeshatoweka,"alisema Nchunga.

Alisema,"suala hilo hivi sasa lipo Polisi na upelelezi unaendelea ili kubaini waliohusika katika kitendo kile."

CHADEMA IKO JUU, CHEZEA MNYIKA WEWE!


John Mnyika,Mbunge wa Ubungo(CHADEMA) aliyeshinda kesi ya uchaguzi.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Ubungo umeunguruma katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika (Chadema) amemshinda tena Hawa Ng'humbi (CCM) baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kutoa hukumu kuwa ushindi wa Mbunge Mnyika uliofanyika Oktoba 31, 2010 ulikuwa wa halali.

Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo akitetewa na Wakili Edson Mbogoro.

Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo iliyoko mbele ya Jaji Upendo Msuya ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi (RO) katika jimbo hilo, (aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni) ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA), Justice Mulokozi.

Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh’umbi alipata kura 50,544.

Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhishwa na matokeo hayo akaamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuyapinga, akimtumia Wakili Issa Maige.

Katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi mahakamani, Ngh’umbi na mashahidi wake walidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kisheria katika ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo ambao umeathiri matokeo hayo.