Tuesday, May 1, 2012


Vicent Company akitupia goli la pekee na la ushindi lililoisambaza Man United


Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Tuliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Weweeeeeee pumbafuuuuuuu

Man City imeichakaza man united bao moja kwa nunge na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, goli la pekee lilifungwa na Vicent Company dakika ya fulani.

AZAM YAILAMBA TOTO

















Patashika nguo kuchanika katika mpambano huo

AZAM imeendeleza wimbi lake la kusaka ubingwa msimu huu baada ya kuichakaza Toto African kwa mabao 3-1 kwenye uwanja Azam Complex Chamazi.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Tchetche alifunga mabao mawili na kumtegeneza la tatu kwa John Boko kabla ya Enyinna Darlington kuifungia Toto bao la kufutia machozi dakika 88.

Kwa ushindi huo Azam sasa imefikisha pointi 56 ikiwa nyuma ya Simba kwa pointi 3 kabla ya mechi ya mwisho zitakazoamua bingwa kwa tofauti ya mabao kama vinara Simba watafungwa na Yanga na Azam watainyuka Kagera Sugar kwa mabao zaidi ya matatu.

Azam waliingia kwenye mchezo huo na kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Kipre Tchetche akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahim Mwaipopo.

Tchetche alifunga bao la pili dakika tisa baadaye akimalizia mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Toto African wakati wakizuia shuti la John Boko.

Kinara wa ufungaji katika ligi msimu huu Boko alipachika bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Tchetche dakika ya 37.

Mabao hayo ya haraka yaliwavunja nguvu mashabiki wanadhaniwa wa Simba waliokodi Daladala na kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kwa lengo la kuishangilia Toto.

Baada ya bao la tatu kocha wa Toto msaidizi Salemain Kigi aliyechukua nafasi ya kocha mkuu Athuman Bilali, alimpumzisha kipa Mustapha Mabrouk na kumwingiza Sunga Ramadhani.

Kocha Bilali anatumikia adhabu ya kadi nyekundu alionyeshwa wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Toto walikuwa wamefika golini kwa Azam mara moja tu kwenye mchezo huo uliokuwa wa upande moja.

Mwamuzi wa mchezo huo alitoa kadi za njano kwa Mrisho Ngasa wa Azam na Ladisraus Mbogo, Emmanuel Swita kwa Toto African.

Uwanja ulifungwa vipaza sauti kila kona na kufunguliwa muziki mkubwa aina ya mchiriki uliokuwa ukiimbwa na kuchezwa na mashabiki wa Azam muda wote wa mchezo.

Kipindi cha pili Toto ilimpumzisha Swita na kuingiaPhabian James huku Azam wakimtoa Mwaipopo na kuingia Abdi Kassim.

Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Toto walirudi mchezoni na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Azam walionyesha kulidhika na mabao yao matatu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Enyinna Darlington alifungia Toto bao la kufutia machozi dakika ya 88 kwa shuti la umbali wa mita 30, lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Mwisho wa mchezo huo kocha wa Toto, Bilali aliangua kilio kudai kujumiwa na kusababisha kufungwa kwao.
Huku wachezaji wa Toto wakitaka kuwapiga viongozi wao pamoja na kipa Mustapha Mabrouk wakiwashutumu kuhusika na kipigo hicho