Wednesday, April 25, 2012

GARI LA KIFAHARI FERRARI ENZO LENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI 1.6 MILIONI LATELEKEZWA DUBAI


Polisi wa Dubai akiingalia Ferrari Enzo iliyotelekezwa Dubai na mtu aliyesadikiwa kuwa ni raia wa Uingereza, habari zaidi zinasema mshkaji huyo alifikia uamuzi wa kusepa na kuacha ndinga yenye mkwanja mrefu baada ya kushindwa kulipa kodi za ndani na kodi za askari wa usalama barabarani.


Ndinga hiyo iliyotelekezwa mwaka jana mwezi wa nane(8) na mchizi huyo, kwasasa serikali ya Dubai imeshatoa amri kwa jeshi la Polisi la nchi hiyo kulipiga mnada, wanahabari wanasema mnada huo haujawahi kutokea katika historia ya minada iliyowahi kufanywa na Polisi kutokana na ukweli kuwa ndinga hiyo ina ya Ferrari Enzo ina thamani ya kufa mtu,kiasi kinachofikia dola za kimarekani milioni 1.6


Habari zinasema kwa Dubai ni kitu cha kawaida kukuta magari ya biashara au ya thamani yakiwa yametelekezwa maeneo ya kuegeshea magari au maeneo ya viwanja vya ndege na wenye mali hizo kusepa kinyemela kukwepa kodi.