Thursday, April 5, 2012

CHELSEA YAIFUATA BARCELONA NUSU FAINALI KLABU BINGWA BARANI ULAYA

Blue is the colour: Chelsea will play Barcelona in the semi-finals of the Champions League
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli la penati alilofunga Lampard

Chelsea imetinga katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuichapa Benfica ya ureno kwa mabao 2-1 na kuipa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya kushinda pia katika mchezo wa kwanza kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali lakini Chelsea ikionekana dhaifu mbele ya Benfica ilifanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika ya 21 kwa njia ya penati baada ya Ashley Cole aliyekuwa akielekea kumsabahi golikipa wa Benfica kuchezewa vibaya katika eneo la hatari,penati hiyo ikitupiwa kambani na Lampard.
Dakika ya 40 Benfica walinyong'onyeshwa baada ya beki wake kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya njano ikiwa ni ya pili na hivyo kutolewa nje.
Benfica kama hawakuwa pungufu vile waliendelea kuwanyanyasa Chelsea na kujipatia bao la kusawazisha katika dakika ya 85 kupitia mshambuliaji wake Jarvia Garcia.
Raul Meireles alieingia kipindi cha pili alihitimisha shughuli katika dakika ya 90 kwa kuachia shuti kali la mbali na kufunga goli zuri katika mchezo huo.
Spot on: Frank Lampard was the match-winner with a penalty in the first half
Lampard akipiga penati iliyoiandikia Chelsea goli la kwanza

Dynamite: Raul Meireles settled the tie beyond all doubt with a thunderous strike into the top corner
Meireles akipigilia msumari wa pili

Dynamite: Raul Meireles settled the tie beyond all doubt with a thunderous strike into the top corner
Mfungaji wa goli la pili Raul Meireles akiwasherehesha mashabiki wa Chelsea

Benfica's Javi Garcia (L) Scores
Javi Garcia akifunga goli maridadi kwa kichwa na kuisawazishia Benfica


Torres alicontrol mpira mbele ya beki wa Benfica