Wednesday, April 4, 2012

Bob Junior-Nichum

MKE WA MAJID MICHEL AMEIONA HII? MAJID NA MERCY JOHNSON

Woow ninatamani na mimi niwe mcheza filamu kwa sababu hiyo ya kubambiabambia mademu wakali,aaah....Hii tasnia inavutia sana!Tukirudi katika mada najiuliza mke wa Majid Michel yuko wapi aione hii ili Majid atakaporudi amzabe vibao,Mercy Johnson ana umbo la kuvutia kimahaba lenye kuweza kusimamisha turubai muda wowote na hiyo ndio utajua kwanini Majid anastahili kupigwa na mkewe.
Pamoja na hayo ni filamu lakini ukaribu huu unaweza kumfanya mke wa Majid akajikalia nyumbani akiwaza huku michozi ikimtiririka mithili ya chemchem ya Udzungwa, pia najiuliza Mercy ameolewa? vp mumewe au mchumba wake anapoyaona haya? Tazama mwenyewe sitaki ushahidi mie........

Mercy Johnson And Majid Michel
Mercy Johnson na Majid Michel

Mercy Johnson And Majid Michel

Mercy Johnson And Majid Michel

Mercy Johnson And Majid Michel
Mercy Johnson na Majid katika pozi tofauti nadhani umejionea mwenyewe kama mmojawapo mpenzi wake anaangalia mara kwa mara anaweza kupatwa na preshaaaa!!!!

BARCELONA NI NOMAA, YAITUPA AC MILAN NJE NA KUTINGA NUSU FAINALI KLABU BINGWA ULAYA

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Andre Iniesta(8) akitupia kambani msumari wa tatu na wa ushindi

Barcelona ya Uhispania imefanikiwa kuingia hatua nzuri katika michuano ya klabu bingwa ya ulaya baada ya kuichapa AC Milan ya Italia kwa magoli 3-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Nou Camp.
Barcelona waliokuwa wakishambulia tangu mwanzoni mwa kipindi iliwachukua dakika 11 pale Leonel Messi alipoangushwa katika eneo la hatari na bila ajizi refa wa mchezo huo aliamuru ipigwe penati, Leonel Messi alitupia penati hiyo kimiani na kuwafanya Barca kuongoz kwa goli moja.
Goli hilo liliwapa ari na kuwanyong'onyesha AC Milan kabla ya kuwarudisha katika mchezo ikiwa ni dakika ya 32 pale mshambuliaji Machachari mbrazil Robinho kufanya kazi ya ziada na kumpatia pasi murua Ibrahimovic nae bila ajizi akamchomekea pande la mwisho Antonio Nocerino akiwa katika nafasi nzuri nae akatupia kambani kuisawazishia AC Milan na kufanya magoli kuwa ni 1-1.
Ilionekana kama AC Milan wamerudi mchezoni kwa kucheza kwa kasi huku Barcelona wakicheza mchezo wao wa kawaida wa pasi nyingi na fupifupi. Kwa mara nyingine tena Barcelona walipata penati nyingine baada ya Nesta kumdandia mtu wakati kona inachongwa kuelekezwa langoni mwa AC Milan.
Dakika ya 53 Andre Iniesta alitupia kambani goli la tatu na kuwakata kabisa maini na kuwafanya AC Milan kuondokana na ndoto za kutinga nusu fainali za klabu bingwa ulaya. Mpaka mpira unakwisha matokeo yalikuwa Barcelona 3-1 AC Milan na hivyo Barcelona kusonga nusu fainali kwa jumla ya mabao 3-1 ikumbukwe mechi ya kwanza iliyochezwa huko Italia timu hizo zilitoshana nguvu.
Tazama picha za matukio katika mechi hiyo
Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Messi akikatiza katika msitu wachezaji wa AC Milan Mexes,Nesta na Nocerino

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Dan Alves akiwa chini na golikipa wa AC Milan Abbiati huku Nesta akiwatazama katika purukushani hiyo

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Fabregas akipimana ubavu na Ambrosini

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Mtu tatu Mexes,Nesta na Nocerino zikimuandama Leonel Messi

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Cuenca akikosa goli la wazi mbele ya Kipa wa AC Milan

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Wachezaji wa AC Milan wakishangilia baada ya Nocerino kutupia goli la kusawazisha

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Messi akifunga penati huku golikipa Abbiati akichumpa bila mafanikio

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Shangwe na chereko baada ya Messi kutupia kambani kwa penati

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Alves akimtuliza mizuka Robinho....take it esy meeeeeen!!!

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Valdes akidaka mpira kichwani mwa Ibrahimovic

Soccer - Barcelona v AC Milan Champions League - Quarter Finals - Second Leg - Nou Camp
Kocha wa AC Milan Allegri akitoa maelekezo ambayo yaligonga mwamba kwa kuchapwa 3-1

Eto'o aipotezea Barcelona