Saturday, March 31, 2012

WEMA AMWAGA CHOZI KWA KUTOLEWA NISHAI NA DIAMOND UKUMBINI KATIKA SHOW KALI MLIMANI CITY











Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.











Diamond akitema cheche katika tamasha hilo














Diamond akitia mbwembwe mbele ya mashabiki wake














Dancers wakimpa support Diamond kufanya makamuzi










Sehemu ya umati wa mashabiki waliohudhuria show hiyo













Diamond akiendeleza makamuzi mbele ya mashabiki











Diamond anazidi kuwapagawisha mashabiki











Songombingo lilianzia pale Dimond aliposhuka stejini na kwenda kwenye meza waliyokaa wakina  Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo walipompa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa udadavuzi wa mambo wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.













Kazi ikaanza Mboni Masimba anamvalisha T'shirt yenye picha ya mpenzi mpya wa Diamond Steve Nyerere anatunza














Mhh........shabiki huyu akimtunza Diamond Dola za kimarekani watu vinywa wazi kulikoni?












Baada ya kutunza dolare za kutosha akaachia tabasamu nene














Wema nae akanyanyuka kwenda kutunza na pesa zikakataliwa














Wema kaganda akilazimisha Diamond apokee zile pesa bila mafanikio..ndio kwanzaaa kidume kiko bizeeeee!!!!!












Baada ya Diamond kugoma kutunzwa na Wema,Wema aliondoka stejini kwa hasira mithili ya Simba aliejeruhiwa









'Michuzi' aliyoikataa Diamond ikiwa stejini haijui iende wapi....













Hapo sasa 'Nimpende nani' uwanjani














Mlimbwende Jokate Mwegelo akijiachia na mashostito zake.














Diamond akimwaga mauno katika meza aliyokaa Jokate
















Mwanadadafada Mboni Masimba akiwa ametinga T'shirt yenye picha ya kifaa kipya cha Diamond














Baadhi ya wadau walimuita mshereheshaji wa show hiyo Taji Liundi akambembeleze Diamond aende kumuomba msamaha Wema lakini Diamond akasema 'nope'













Diamond akijiachia na warembo













Mashosti wakijaribu kumbembeleza Wema aache kulia kwani hayo yote ni ya dunia














Duuuh..Wema akizidi kumwaga chozi!
"sitakiiiiiiiiiiiii aaaaaaaaaaaaaaaaah aaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhh wakunifanyia hivi mimi jamani aaaaaaaaaaaaaaaaah aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah diamond diamond aaaaahhh aaaaaahhhhhh!!















Ommy Dimpoz akitoa ushuhuda walipotokea na Diamond














Ushuhuda ulimgusa Diamond na kumwaga chozi "mhmhhmmmmmm"














Amini na Barnaba wakimpa shavu Diamond katika show hiyo.
















Hatimae Wema atuliza machungu kwa kumtunza Barnaba! "chukuaaa si anajifanya mjanja ataona akinitaka tena simtaki"


JOHN BOKO"ADEBAYOR" ACHOKA KUZOMEWA ASEMA 'STARS SASA BAAAAAAAASSSS'


JOHN BOKO 'ADEBAYOR'

Kinara wa mabao katika historia ya klabu ya Azam FC na kinara wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom inayoendelea, John Raphael Boko 'Adebayor' ameliandikia barua shirikisho la soka nchini TFF ya kustaafu kuichezea timu ya Taifa 'Taifa Stars'. Huku akimuacha njia panda kocha wa kikosi hicho Jan Poulsen.

Boko amefikia uwamuzi huo kutokana na kuchoshwa na tabia za mashabiki wanao hudhuria mechi za Timu ya Taifa kumzomea kila anapopagwa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook unasema kuwa Boko amewaomba TFF walikemee suala la wachezaji kuzomewa wakiwa na jezi ya Taifa.

"John Boko astaafu kuchezea timu ya taifa na sasa anaelekeza nguvu zake kwa timu yake ya Azam FC, kwa mujibu wa barua yake kwa TFF Boko amewaomba viongozi wa soka nchini kukemea tabia ya zomea zomea Kama walivyokemea uharibifu wa Mali za uwanja," ili eleza taarifa hiyo.

Katika blog ya Shaffih Sports imemnukuu Boko akisema; "Nimefikia maamuzi haya baada ya kufikiria sana, nimekuwa nikijitoa kwa hali na mali kulitumikia taifa langu lakini mashabiki wa timu yetu wanaona sifai, hivyo ni bora nijitoe au nistaafu kuichezea timu hiyo ili kuepekana na dhahama zao. Naitakia kila kheri timu yangu ya taifa naipenda na nitaendelea kuipenda siku zote."

Boko ni miongoni mwa washambuliaji bora nchini kwa kizazi hiki, na amekuwa chaguo la Poulsein toka aachane na washambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa madai ya kwamba hawajitumi wakiwa na timu ya Taifa.

Kama Poulsein akiendelea na uwamuzi wake wakutowajumuisha washambuliaji hao wa TP Mazembe, ni wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu katika kusaka washambuliaji watakao ziba mwanya huo.

LIGI KUU TANZANIA BARA NYASI KUTOA 'JASHO' LEO SIMBA Vs LYON, YANGA Vs COASTAL UNION


Kocha wa Simba S.C Milovan Cirkovic.

Mbilingembilenge za ligi kuu Tanzania bara zinaendelea leo ambapo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, mabingwa watetezi Yanga watakakuwa wageni wa Coastal Union, huku vinara wa ligi Simba wakiwa na kazi mbele ya African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania, timu za Simba na Yanga watashuka dimbani wakiwa na malengo tofauti kila mmoja, Yanga wenyewe wanajua kupoteza mchezo huo ni kupoteza ndoto yao ya kutetea ubingwa wao huku Simba wakitaka ushindi wajiimarishe kileleni kabla ya kuelekea Algeria kuivaa ES Setif.


Kocha wa Yanga Kostadin Papic.

Yanga hivi sasa inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43, hivyo ushindi dhidi ya Coastal utasaidia kupunguza pengo kati yake na kinara Simba inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 47, pia kuiondoa Azam FC katika nafasi ya pili ambayo ina pointi 44 kabla ya mechi yake ya kesho dhidi ya Ruvu JKT.

Ukweli ni kwamba uzito wa mechi kati ya Yanga na Coastal Union unazidishwa na taswira tofauti za timu zote mbili hivi sasa pamoja na uwepo wa kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio'.

Mabingwa hao wa mwaka 1988, Coastal Union waliojikusanyia pointi 29 baada ya kuzinduka na kushinda mechi sita mfululizo za raundi ya pili wenyewe wanatarajiwa kuendeleza rekodi hiyo kwa kusaka pointi tatu zitakazoipandisha juu kutoka katika nafasi ya sita iliyojiweka mpaka sasa.

Kocha wa Coastal, Kihwelo 'Julio' ameapa kuwadharirisha wapinzani wake kwenye mchezo huo akitarajiwa kuwatumia nyota kama Benard Mwalala, Edwin Mukenya kufikia malengo yake ingawa pia yupo Aziz Gilla anayecheza hapo kwa mkopo akitokea Simba.

Naye kocha wa Yanga, Kostadin Papic bila shaka ataingiza timu uwanjani akiwa katika hali ya kujiamini baada ya nyota wake waliokuwa kifungoni kufunguliwa kwa muda hivyo itakuwa ni hiyari yake kuwatumia au la.

Silaha za Papic zinazoweza kuonekana leo baada ya kunasuliwa kwa muda kutoka katika kifungo cha Kamati ya Ligi kutokana na utovu wa nidhamu ni mabeki, Nadir Haroub na mwenzake Stephano Mwasika, pamoja na viungo Omega Seme, Nurdin Bakari na mshambuliaji Jerryson Tegete.

Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma ambaye atasaidiwa na Rashid Lwena (Ruvuma) na Issa Malimali (Ruvuma).

Vita nyingine itakuwa jijini Dar es Salaam, wakati vinara wa ligi Simba wakiwa kwenye kiwango bora zaidi watakapowakabili ndugu zao African Lyon.

Kocha Milovan Cirkovic amewasisitizia wachezaji wake kutofanya uzembe utakaotoa nafasi kwa wapinzani wao ili kujiweka vizuri kabla ya kuivaa ES Setif wiki ijayo.

Simba itashuka dimbani bila ya kiungo wake Patrick Mafisango aliyesimamishwa na uongozi kutokana na utovu wa nidhamu.

Hata hivyo, Cirkovic licha ya kuwa na akiba ya kutosha ya wachezaji mahiri pia atakuwa na furaha baada ya kurejea kwa beki aliyekuwa majeruhi Juma Jabu.

Kesho matajiri wa Chamazi, Azam watakuwa wenyeji wa Ruvu JKT timu iliyopoteza makali yake katika siku za hivi karibuni.