Wednesday, March 28, 2012

VICHUPI VYAPIGWA 'STOP' MASHINDANO YA OLIMPIKI 2012


Vichupi vilivyopigwa "stop"olimpiki

Wanawake sasa hawatohitajika kuvaa vichupi'bikini"katika mchezo wa volleyball ya ufukweni katika mashindano ya olimpiki yatakayofanyika katika jiji la London nchini Uingereza mwaka huu.
Utaratibu huo mpya umetangaza siku ya jumanne 27 March 2012 na kamati ya maandalizi ya Olimpiki ukisema kuwa katika mashindano ya Olimpiki ya kipindi cha kiangazi kwa upande wa mchezo wa Volleyball wanawake watatakiwa kuvaa kaptula fupi ama sketi fupi"vibwaya".
Tangu mashindano ya Olimpiki yalipoanzishwa mwaka 1996 huko Atlanta wanawake wamekuwa wakivaa vichupi"Bikini" na sasa hawatoruhusiwa tena kuvaa vichupi wanaruhusiwa kuvaa kaptlula ama sketi fupi pia "body suit".
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuweza kuenda sambamba na tamaduni za nchi mbalimbali zinazoshiriki michezo ya olimpiki. Kaptula ama sketi fupi zenye urefu wa nchi 1.18 juu ya magoti au bodysuit ndio mavazi yatakayoruhusiwa kwa mujibu wa utaratibu mpya wa kamati ya maandalizi ya olimpiki.
Kamati hiyo imesema utaratibu huu mpya utasaidia kushawishi nchi zenye tamaduni tofauti kukutana pamoja bila migongano.

Uwanja unapogeuka dimbwi la matope


Mbwana Samatta kushoto na wachezaji wengine wa TP Mazembe na timu pinzani wakiwa wametapakaa matope baada ya mvua kunyesha na kubadili hali ya uwanja wa Soka huko jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC).

Mbwana Samatta"Samagoal" atupia kambani aumia bega nje siku 10


Samatta akitolewa uwanjani na machela baada ya kuumia bega katika mechi dhidi ya Power Dynamos

MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe, Mbwana Samata atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku baada ya kuteguka bega la mkono wa kushoto.Samata aliteguka bega hilo wakati timu yake ya TP Mazembe ya DR Congo ilipokuwa ikicheza dhidi ya timu ya Power Dynamos ya Zambia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye uwanja wa Arthur Davies mjini Kitwe, Zambia.


Samatta akiwatoka mabeki wa Power Dynamos

Mshambuliaji huyo kijana ambaye mashabiki wa TP Mazembe wanamuita 'Samagoal' aliumia wakati alipokuwa akitaka kufunga bao, ambapo aliangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Dyanamos, lakini mwamuzi hakutoa penati wala kadi nyekundu.

Kutokana na kuumia huko katika dakika ya 61, Mbwana Samata alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Deo Kanda.Hivi sasa Samata yupo katika hospitali ya TP Mazembe akifanyiwa uchunguzi zaidi baada bega hilo kuendelea kumsumbua, ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10.

Katika mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa matokeo ya bao 1-1, bao la TP Mazembe lilifungwa na Mbwana Samata katika dakika ya 16, huku mchezaji huyo akiwa anaifungia bao TP Mazembe katika kila mechi anayocheza na akiwa na uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

 

CHELSEA,REAL MADRID ZACHUNGULIA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Solomon Kalou akitupia kambani goli pekee na la ushindi wa Chelsea dhidi ya Benfica

Bao la Salomon Kalou iliisaidia timu ya Chelsea kuingiza mguu mmoja katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mabinwa barani ulaya baada ya kuwachapa wenyeji wao Benfica ya Ureno.
Mwamba huyo wa Ivory Coast alifunga bao hilo la pekee katika daikia ya 75 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Fernando Torres ambaye nae katika mechi hii alikuwa katika hali nzuri.
Hapo awali Kalou alipoteza nafasi kadhaa za kufungo mabao.
Kauli ya Drogba iliyodaiwa awali na kocha wa Benfica kuwa ilikuwa ya kejeli kwa timu yake na kutaka kauli hiyo ijibiwe kwa kipigo kwa Chelsea, goli la Kalou lilionekana kuipa nguvu zaidi kauli hiyo na huenda hata kocha mwenyewe Jorge Jesus ameumia zaidi kwani dhamirra yake ya kuwaadhibu Chelsea haikutokea.
Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo katika kuhakikisha anapata ushindi, aliwatumia wachezaji wake wenye uzoefu mkubwa na uchezaji wa timu za Ureno.
Wachezaji wa zamani wa Benfica kama vile kina David Luiz, Ramires, Raul Meireles na Paulo Ferreira ndio waliopewa kibarua cha kuihangaisha timu yao ya zamani.

Katika robo fainali nyingine  Real Madrid wameinyanyasa Apoel ya Nicosia kwa kuishushia kipigo cha mabao matatu kwa bila nyumbani kwao.

Kaka akishangilia baada ya kutupia kambani goli la pili

Alikuwa Kaka kiungo mshambuliaji akitokea benchi, ndiye aliyechochea ushindi huo dhidi ya Apoel ambao waliikatalia Real Madrid kufunga bao hadi kipindi cha pili.
Ilikuwa ni krosi ya Kaka kwa Karim Benzema iliyozaa goli la kwanza na Kaka naye akipokea krosi ya Marcelo kufunga goli la pili na Benzema akikamilisha karamu ya magoli kwa Real Madrid kwa kufunga goli la tatu akipokea pasi maridadi ya Mezut Ozil.