Tuesday, March 27, 2012

GOAL OF THE WEEK

ZLATAN IBRAHIMOVIC - AC MILAN Vs ROMA

NITAREJEA-Diamond ft Hawa

HAOOOO-Mwasiti ft Chid Beeeeeenz

Man United yaichapa Fulham yang'ang'ania kileleni

Mshambulizi mwenye misuli Wayne Rooney alihakikisha timu yake Manchester United inapanda kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza kwa kuichapa Fulham bao moja bila.
Rooney na Evans wakishangilia goli

Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea pasi safi kutoka kwa Jonny Evans.
Kwa ushindi huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu.
Kufikia sasa timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.
Manchester City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland.
Vijana hao wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn.
Hata hivyo mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti.
Hii ni baada da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha mshambulizi Danny Murphy katika eneo la hatari katika dakika ya 87.
Man United 1-0 Fulham

meneja huyo wa Fulham amenukulikwa akisema kuwa kila mtu aliyeshuhudia mechi hiyo alitarajia wapewe penalti.