Tuesday, March 20, 2012

UGONJWA WA MOYO TISHIO KWA MAISHA YA WACHEZAJI


Fabrice Muamba ambaye hali yake sio nzuri hospitalini baada ya kuanguka uwanjani na kuzirai kutokana na mshituko wa moyo

Wachezaji na refa wakiomba msaada baada ya Muamba kuanguka na kuzirai

Bale akimnyamazisha Defoe kulia wakati Muamba alipoanguka na kuzirai

Watu wengi wanafahamu kuwa matatizo ya moyo hasaa mshtuko wa moyo yanaweza tu kuwapata watu wazee.
Lakini kuna takriban vifo miatano huripotiwa kila mwaka nchini Uingereza kutokana na watu walio chini ya umri wa miaka 30.
Wakati ikitokea ni picha ya kushtua. Hasa hasa inapotokea kwa nyota wa michezo kama Fabrice Muamba mwenye umri wa miaka 23 pekee.
Fabrice ni mmoja wa wachezji walio na afya nzuri zaidi katika kilabu chake, Bolton Wanderers.
Matamshi sawa na hayo yalitolewa kuhusu marehemu Marc-Vivien Foe, aliyekuwa mchezji wa Cameroon.
Marc-Vivien alianguka na kupoteza fahamu, wakati wa mechi ya kimataifa mwaka 2003.

Marc Vivien Foe enzi za uhai wake

Marehemu Foe siku alipoanguka na kuzirai na kuwa ndio mwisho wa maisha yake

Foe akitolewa nje na machela siku alipozirai na kupoteza maisha uwanjani

Lakini kinachosababisha vifo kama hivi huwa sana kutokana na mtu kurithi ugonjwa fulani kuliko hali ya kiafya ya mtu.
Hitilafu katika celi za mwili ndio chanzo kikubwa cha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au ugonjwa wa misuli ya moyo ujulikanao kama "Cardiomyopathies".
Inawezekana hali ya mtu inaweza kumfanya kupata mshituko wa moyo, licha ya kuwa anafanya mazoezi kila siku na wala hasongwi sana na mawazo. Hii ni kwa mujibu wa Daktari mmoja mtaalamu wa matibabu ya moyo Leonard Shapiro.
Sasa inawezekana vipi mtu mwenye kufanya mazoezi moyo wake kusimama? Hili kwa kweli halijulikani vyema. Lakini utafiti unapendekeza kuwa wale waliorithi matatizo ya moyo uwezekano wa moyo wao kusimama ni mara mbili sawa na wale wanaoshiriki michezo inayohitaji nguvu nyingi.
Daktari Leonard Shapiro, ambaye ni mtaalamu wa matibabu ya moyo pamoja na kuwa mshauri wa shirikisho la soka Uingereza, FA, anasema ni vigumu kufahamu chanzo cha mshituko wa moyo.
Lakini anasisitiza kuwa kuna mambo kadhaa yanayoweza kumfanya mtu kupata mshituko wa licha ya kuwa anajihusiha sana na mazoezi yanayohitaji nguvu nyingi.
Sasa je , nini kinaweza kufanyika ili kuzuia matukio kama haya?
Vitengo mbali mbali vya michezo nchini Uingereza hufanyia wachezaji uchunguzi wa kiafya, ingawa sio lazima, kama ilivyo katika baadhi ya nchi , mfano Italy.

Katika soka, wachezaji hufanyiwa uchungizi wa kiafya wakiwa na umri wa miaka 16 na kisha kupata ukaguzi zaidi katika siku za baadaye.
Wengi wanaopatikana kuwa na matatizo yoyote, huwa hawaruhusiwi kushirki kwenye michezo ya hali ya juu.
Daktari wa moyo katika michezo, Sanjay Sharma, anasema kuwa ukaguzi huo ni wa kiwango cha juu lakini sio kamili.
Ukaguzi wenyewe unahusu kuchukua historia ya kiafya ya mchezaji kuhusu maradhi ya moyo, kufahamu ikiwa mchezaji huhisi uchungu kifuani wakati akipumua na hata kuuliza maswali kuhusu historia ya familia kwa sababu matatizo mengi ya moyo hutokana na kurithi.
Hata hivyo ukaguzi huu sio hakikisho kuwa mchezaji hawezi kuwa matatizo ya moyo baadaye na tatizo kubwa zaidi huwa matatizo hayo huwa sio ya kudumu.
Hujitokeza tu na kisha kutibika, sawa na hali ya Muamba. Imesemekana kuwa Muamba amefanyiwa ukaguzi wa moyo mara nne tangu aanze kucheza soka, wa hivi karibuni ukifanywa mwaka jana