Monday, March 5, 2012

SIMBA DUME LA MBEGU OKWI,SUNZU,KASEJA WANG'AA


Felix Sunzu (kushoto) akitupia kambani goli la kwanza la Simba huku kipa na beki wa Kiyovu wakigaragara bila mafanikio

Magoli ya Mzambia Felix Sunzu katika dakika ya 19 na 32 yametosha kuifanya Simba kusonga mbele. Magoli yote yakiwa yametokana na juhudi binafsi za mshambuliaji machachari Emanuel Okwi. Kiyovu walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 77 kupitia kwa mshambuliaji wao Neli, Goli hilo liliwapa nguvu Kiyovu na kutaka kuongeza goli zaidi. Kama Kiyovu wangesawazisha, basi Simba wasingeweza kusonga mbele.

Mashabiki wa Simba wakishangilia bao

Simba ambayo beki yake haikuwa makini sana, ingawa waliweza kufanya maajabu kama yaliyotokea. Shukurani pia ziende kwa Kaseja ambaye kama sio jitihada zake za kuokoa michomo mikali kutoka kwa washambuliaji wa Kiyovu katika dakika za nyongeza basi tungekuwa tunaongea mengine.

Emmanuel Okwi (kulia)ambaye alikuwa mwiba mkali kwa Kiyovu katika mechi hiyo

Kwa matokeo hayo ni cheko kubwa tu kwa mashabiki na wapenzi wa Simba, huku wakimuacha mtani akiugulia baada ya kichapo cha goli moja kwa buyu kutoka kwa Zamalek huko Misri.
Mchezo uliochezwa huko Rwanda, Kigali Simba na Kiyovu zilitoshana nguvu kwa kwenda sare ya 1-1. Kwa matokeo hayo Kiyovu imetolewa kwa jumla ya magoli 3 - 2. (Simba 3-2 Kiyovu).

MAN UNITED YAENDELEZA MAUMIVU KWA SPURS

Ashley Young akishangilia moja ya mabao yake na Rooney
Ashley Young na Rooney wakishangilia goli

Ashley Young alifunga mabao mawili wakati Manchester United ilipofanikiwa kupunguza wigo wa pointi na kuwa mbili dhidi ya wanaoongoza ligi ya kandanda ya England Manchester City.
Spurs walianza vyema mchezo huo, huku mlinda mlango wa Manchester United David de Gea alikaa imara na kumnyima bao Jake Livermore.
Lakini Manchester United walimaliza mchezo kwa aina yake, Wayne Rooney akianza kufungua lango la Tottenham alipounganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ashley Young kipindi cha kwanza.

Ashley Young akitupia kambani goli la pili la Man United

Young aliweza kufunga mabao mawili kipindi cha pili kabla ya Jermain Defoe aliyeingizwa dakika za mwisho kuifungia Tottenham bao la kufutia machozi.
Katika mchezo mwengine Pavel Pogrebnyak alifunga mabao matatu peke yake wakati Fulham ilipoivurumishia Wolves mabao 5-0 na kumuweka katika wakati mgumu meneja mpya wa Wolves Terry Connor .
Man United 3-1 Tottenham Hotspurs

Mshambuliaji huyo kutoka Urusi alianza kupachika bao katika dakika ya 36 alipounganisha mkwaju wa kona wa Damien Duff kabla ya kuunganisha mpira wa chini uliopigwa na Andy Johnson na kuandika bao la pili kabla ya mapumziko.
Clint Dempsey alifanikiwa kumpiga chenga mlinda mlango wa Wolves Wayne Hennessey na kufunga bao la tatu, kabla ya Pogrebnyak kwa mara nyingine kupachika bao la tatu kwa kuunganisha mkwaju uliopigwa na Johnson.
Na alikuwa Dempsey aliyefunga bao lake la pili na la tano kwa Fulham lililozidi kuichosha Wolves.
Naye Shola Ameobi aliifungia Newcastle bao muhimu la kusawazisha wakati walipokuwa wamebanwa na majirani wao Sunderland, ambao wachezaji wao wawili walitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Nicklas Bendtner alifunga mkwaju wa penalti baada ya Mike Williamson kucheza rafu isiyolazima kwa Michael Turner, na kuipatia Sunderland bao la kuongoza.
Demba Ba alikosa kufunga mkwaju wa penalti kabla ya Ameobi kurejesha matumaini ya Newcastle kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za nyongeza.
Stephane Sessegnon alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Cheick Tiote, wakati Lee Cattermole alikumbana na kadi nyekundu baada ya mpira kumalizika alipooneshwa kadi ya pili ya manjano kwa kumtolea maneo ya kuudhi mwamuzi.

ANDRE VILLAS-BOAS "AVB" APIGWA CHINI CHELSEA


Kocha aliyetimuliwa Andre Villas-Boas kushoto na kulia kocha anayeshikilia timu kwa sasa Roberto Di-Matteo

Klabu ya Ligi kuu ya England, Chelsea ni kwamba klabu hio imeachana na kocha Andre Villas-Boas leo jumapili.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 amepoteza kazi hio saa 24 baada ya kupoteza jana pambano la Ligi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0.
Kufuatia mechi ya jana Chelsea ilijikuta katika nafasi ya tano kweenye msimamo wa Ligi.
Tangazo la Chelsea limesema kua aliyekua naibu wa Kocha huyo Roberto Di Matteo atashikilia wadhifa wa Kocha hadi mwisho wa msimu.
Villas-Boas, aliwasili uwanja wa Chelsea kutoka Porto mwezi juni mwaka 2011, na ametimuliwa kwa matokeo yasiyo ridhisha yaliyoiacha Chelsea katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi, hali ambayo inaiweka klabu hio ukingoni kukosa kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya mwakani. Pamoja na hayo Chelsea ilichapwa 3-1 dhidi ya Napoli.
Kocha huyo inasemekana alijenga uhasama baina yake na wachezaji wakuu katika klabu ya Chelsea, akiwemo kiungo Frank Lampard na vilevile mfululizo wa matokeo mabovu akiweza tu ushindi mara moja katika mechi saba.
Matokeo haya hasa ndio yaliyosababisha mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich kumchukulia hatua.
Msumari wa mwisho ulitokea jumamosi baada ya Chelsea kupoteza mechi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0 kupitia Garth McAuley.
Taarifa ya bodi ya Chelsea iliyotangaza kuvunjika kwa ndoa kati ya Chelsea na Villas Boas, imesifu juhudi zake na kusikitika kua hawakuweza kudumu zaidi ya hapa kutokana na matokeo mabovu na kukosekana kwa dalili kua hali hio inaweza kubadilika.
Villas Boas aliletwa Chelsea kubadili kikosi kichovu baada ya ushindi wake wa vikombe vinne akiwa na klabu ya Porto msimu uliopita, lakini mda wake na Chelsea uligubikwa na habari za mvutano kama ulioarifiwa na Ma meneja waliomtangulia kua ndio uliosababisha kushindwa kuiongoza Chelsea na hivyo kutimuliwa.

ARSENAL YALIPA KISASI KWA LIVERPOOL YAICHAPA 2-1


Van Persie katikati,Vermaelen(5) na Walcott kulia wakishangilia goli la pili la Arsenal

Bao la ushindi la Mshambuliaji Mholanzi Robin van Persie"R.V.P" katika muda wa nyongeza, limeipatia Arsenal ushindi wa ajabu na kuwaacha nyuma Liverpool kwa tofauti ya pointi 10 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwenye heka heka za kuwania nafasi nne bora za juu.
Liverpool walitawala mchezo kwa muda mrefu, lakini Dirk Kuyt alikosa nafasi nzuri ya kufunga kwa mkwaju wa penalti baada ya kuokolewa mara mbili na mlinda mlango wa Arsenal, na vile vile mkwaju wa Luis Suarez nao kukosa kulenga lango na kukonga mlingoti wa lango.

Arsene Wenger

Hatimaye Liverpool walifanikiwa kuongoza wakati mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny alipojifunga mwenyewe alipokuwa katika harakati ya kuokoa mkwaju wa pembeni wa Jordan Henderson.
Lakini Arsenal hawakuzubaa na iliwachukua muda mfupi kipindi cha kwanza kusawazisha kwa bao la Van Persie kwa kichwa na akafanikiwa tena kufunga bao la pili katika dakika za nyongeza kipindi cha pili baada ya kunyanyuliwa mpira wa juu na Alex Song.
Liverpool sasa wanakabiliwa na kibarua kigumu kuweza kumaliza katika nafasi nne za juu, kwani kwa matokeo hayo bado wanaendelea kubakia nafasi ya saba wakiwa na pointi 39, huku Arsenal wakijichimbia katika nafasi ya nne na sasa wamefikisha pointi 49.

PUTIN AVUA UWAZIRI MKUU AVAA URAIS URUSI


Putin na Medved rais aliemaliza muda wake nchini Urusi

Waziri Mkuu Vladimir Putin ametangaza kuwa ameshinda uchaguzi wa Urais wa Urusi.
Matokeo ya awali yanampa Putin ushindi wa asilimia 60.
Hii inamaanisha kuwa Vladimir Putin anarudi tena kama rais kwa kipindi cha tatu baada ya kuhudumu kama waziri Mkuu wa Urusi.
Kiongozi huo aling'atuko toka kiti cha urais mwaka 2008 baada ya kuhudu kwa mihula miwili kwa mujibu wa katiba ya Urusi.
Putin aliwaambia maelefu ya wafuasi wake kuwa wameshinda katika uchaguzi uliokuwa huru na wa wazi.
Akiandamana na Rais wa sasa wa Urusi ,Dmitry Medvedev kiongozi huyo aliwashukuru wafuasi wao walio kote nchini kwa kujitokeza na kumchagua tena kama rais wao.
Lakini makundi ya upinzani yamedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na kuwa eti kuna baadhi ya watu waliopiga kura mara mbili.
Viongozi hao wa upinzani wametaka watu wajitokeze barabarani kuanzia jumatatu kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo