Tuesday, February 7, 2012

Mechi ya Yanga kuhamishiwa Sudan ni sawa na kuruka maji na kukanyaga matope


Wapiganaji wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan

Sehemu ya uwanja ikiungua baada ya kutokea vurugu kati ya mechi ya Al-ahly dhidi ya Al-masry nchini Misri

Mechi ya Yanga na Zamalek kuhamishiwa Sudan kutoka Misri kutokana na vurugu zilizotokea Misri na kuua mashabiki uwanjani, Uamuzi huo ni sawa na kuruka maji na kukanyaga matope.
Kama timu zinahofia kucheza Misri kutokana na kuhofia usalama wao sidhani kama Sudan ni sehemu salama, kwani hivi sasa Sudan kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe na mgogoro mkuu ukiwa ni mafuta yanayopatikana katika mipaka ya Sudan kusini na Khartoum,huku serikali mbili zikishutumiana kila moja ikimhofia mwenzake kuwasaidia waasi wanaosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo, Sudan inaweza kuwa si sehemu salama sana kwani mwaka 2009 wakati wa mechi ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2010 iliyozikutanisha Misri na Algeria kulitokea vurugu na mamia ya mashabiki kujeruhi.

Liverpool yatoa yatoshana nguvu na Tottenham,kuivaa Man United Jumamosi

Bale wa Tottenham akijaribu kuwahadaa walinzi wa Liverpool

Liverpool imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Spurs wakicheza bila ya wachezaji wao wengi na pia bila ya meneja wao Harry Redknapp, walicheza kufa na kupona kuzuia mashambulizi ya Liverpool yaliyokuwa yakiongozwa na Andy Carroll.

Paka akikatiza uwanjani katika mechi ya Liverpool na Spurs,ingekuwa bongo ungesikia shutuma za uchawi.

Luis Suarez aliingia muda mchache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kupata nafasi nzuri, lakini kipa wa Spurs Brad Friedel aliudaka mpira.
Liverpool sasa wanasalia katika nafasi ya saba wakiwa na pointi 39 pointi moja nyuma ya Arsenal. Spurs wamefikisha pointi 50, pointi saba nyuma ya Man City wanaoongoza ligi, na pointi tano nyuma ya Man United waliopo katika nafasi ya pili na pointi 55.
Liverpool watapambana na United Jumamosi.
Paka akikatiza uwanjani