Thursday, November 17, 2011

Onesho la sanaa ya matikiti maji yafana(Water melon art Festival)

Wengi tunayafahamu matikiti maji ama kwa lugha ya kigeni WATERMELON.
Huko nchini Italia kuna maonesho yanayojulikana kama Watermelon art Festival, ambapo wasanii kutoka sehemu mbalimbali za Italia hukutana huku kila mmoja akiwa na matikiti kadhaa ambayo ametumia usanii wake kuyatia nakshinakshi za aina mbalimbali na kuleta maumbo tofauti yenye kuvutia.Zifuatazo ni baadhi ya picha za maonesho hayo huko Italia.





















Syria "kimenuka" Jumuiya ya nchi za Kiarabu yaipa siku3 kumaliza Mzozo

Raia waendelea kujeruhiwa
Mmoja wa majeruhi akipata huduma ya kwanza

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe anatarajiwa kufanya ziara maalum nchini Uturuki, kujadili hatua dhidi ya mzozo unaoendelea nchini Syria.

Jumuiya ya nchi za kiarabu imeipa Syria siku tatu kumaliza tatizo hilo la sivyo itawekewa vikwazo vya kiuchumi.

Mmoja kati ya waandamanaji nchini Syria akiwa amebeba bango"Bashar acha mauaji"
Habari zinasema majeshi yaliyoasi yameendelea kulenga kambi za jeshi linalotii serikali.
Ni miezi minane ambapo waandamanaji wasiokuwa na silaha wamekuwa wakilengwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar Assad. Hali imebadilika na majeshi asi yameanza kukabiliana na mahasimu wao.


Rais wa Syria Bashar Al-asaad

Duru kwamba majeshi yaliyoasi na chini ya mwavuli Jeshi Huru La Syria yameshambulia vituo kadhaa vya kijeshi mjini Damascus na kuwaua wanajeshi kadhaa wa serikali ya Syria bado hazijathibitishwa. Lakini ikiwa madai haya yana ukweli wowote, basi ni ishara kwamba huenda mzozo wa Syria umechukua mkondo hatari.

Jumuiya ya nchi za kiarabu imeonya kuiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi ikiwa serikali ya Rais Assad haitakoma kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na imetaka dhuluma hizo kukomeshwa siku tatu.


Maandamano nchini Syria kupinga utawala wa Bashar


Umati wa waandamanaji nchini Syria

Ututruki pia inatathmini kuiwekea Syria vikwazo. Tayari Marekani na jumuiya ya Ulaya zimeweka vikwazo, japo haijabainika athari za viwazo hivi ni ipi.

Jumuiya ya nchi za Magharibi na mataifa ya magharibi yameanza kutafakari mustakabali wa Syria bila uwongozi wa Bashar Al Asaad.



Waandamanaji nchini Syria

Hata hivyo pande zote ziko maakini kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo. Hata hivyo ni vigumu kuafikia lengo hilo bila kuwepo ung'anganizi wa madaraka usipokuwa kwa mtutu wa bunduki.