Thursday, October 20, 2011

Song of the day, AFRICA UNITE by BOB MARLEY. Dedication to all Gaddafi supporters.

R.I.P MUAMMAR GADDAFI


Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi enzi za uhai wake.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, ameuawa katika mapigano kati ya vikosi vinavyomtii na vile vya Baraza la Mpito mjni Sirte, akiwa mbioni kuukimbia mji huo.

Wasifu wa Gaddafi
Jina lake kamili ni Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi, alizaliwa tarehe 7 Juni 1942, katika mji wa Sirte, kaskazini magharibi ya Libya
· Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969 na kuondoshwa madarakani na waasi walioungwa mkono na Jumuiya ya Kujihami ya NATO mwaka 2011
· Utawala wake wa miaka 41 unatajwa kuwa wa nne kwa urefu kwa utawala usiokuwa wa kifalme. Alijiita Kaka Kiongozi, Mlinzi wa Mapinduzi na Mfalme wa Wafalme
· Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera kimeripoti kuwa Gaddafi ameuawa tarehe 20 Oktoba 2011 baada ya kukamatwa kutokana na mapigano kati ya walinzi wake na wapiganaji wa vikosi vya Baraza la Mpito linaloongoza sasa Libya





WEZI WATUMIA MBINU ZA FILAMU YA BEN AFFLECK KUIBA MAMILIONI

Image icon
Sehemu ya picha katika filamu hiyo ya THE TOWN

Kuna njia nyingi za kutumia mafunzo yatokanayo na filamu sehemu mbalimbali za dunia, Mafanikio yanayovutia kutumia mbinu zake yaweza kuwa tuzo au umaarufu uliotokana na filamu hiyo, Wakati mwingine huweza kuwavutia watu kufuata yaliyomo katika filamu hizo katika kutimiza ndoto zao maishani na kwa hilo Mwandishi wa filamu ya ujangili iitwayo THE TOWN Ben Affleck anastahili kupewa heshima kutokana na filamu yake hiyo ya mwaka 2010 kushawishi makundi ya watu kutimiza ndoto zao kwa kutumia mbinu zilizotumika katika filamu hiyo kwa kufanya uhalifu na kupora mamilioni ya pesa.
T
ukio hilo limetokea huko New York nchini marekani ambapo kundi la wezi limefanikiwa kufanya uporaji wa kiasi cha dola za kimarekani 217,000 katika matukio 62, ambapo imearifiwa katika matukio hayo hawajavamia benki yeyote maeneo waliyofanya uvamizi na kupata pesa hizo ni maeneo ya biashara za kawaida na mashine za kutolea pesa"ATM".

Haya dunia ina mambo wasiwasi wangu mambo ya kuiga au kutumia mifano ya kwenye filamu isifikie kwenye zile filamu za mauaji ya kikatili kwa maana watu wote watakuwa makatili sana, nadhani kuna haja ya kuwawekea watoto wetu mipaka ya kuangalia filamu kwani ukatili,busara na huruma kwa mtoto ni muendelezo kadri anavyokua,hivyo akizoea kuangalia filamu za kikatili kuna hatari akawa mkatili kwani hisia na matendo yatakuwa yamejengeka akilini mwake.

Barcelona,Arsenal Chelsea zafanya kweli ligi ya mabingwa Ulaya

Chelsea ilipoiadhibu Genk 5-0


Ramsey akitia kambani dakika za majeruhi na kuipaisha Arsenal

WAYDAD NA ESPERANCE USO KWA MACHO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRICA

NYOTA wa Ghana, Harrison Afful anaamini Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu kati ya Esperance dhidi ya Wydad Casablanca itakuwa na uzuri wa aina yake. Beki huyo wa Esperance aliyeongoza ushindi wa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan mwishoni mwa wiki, huku Wydad ikisonga mbele kwa fainali kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Enyimba.

"Wydad ni timu nzuri. Wanatumia nguvu na akili na wanacheza soka nzuri kama tunavyofanya sisi," alisema Afful.
"Kwa hiyo itakuwa ni mechi nzuri ambayo kila moja atapenda kuitazama."

Esperance ambauo mwaka jana ilikosa ubingwa baada ya kufungwa na mabingwa wa DR Congo, TP Mazembe haijawahi kutwaa ubingwa huo wa Afrika tangu kuanzisha kwa Ligi ya Mabingwa kutoka kwenye mfumo wa Kombe la Washindi mwaka 1997.

Timu hiyo ya Tunisia imeshacheza na wabeba hao wa Morocco kwenye hatua ya makundi katika mashindano ya msimu huu.Mwezi Agosti wakiwa katika Kundi B mechi iliyofanyika Casablanca ilimalizika kwa sare 2-2, wakati ile ya marudiano jijini Tunis hawakufungana.

"Tumecheza mara mbili dhidi yao, hivyo kila moja anamjua vizuri mwenzake," alisema Afful. "Kwa kuzingatia malengo yetu ni umoja, tunaweza kufanya kile tunachotaka kuchukua ubingwa."

Wydad, imefuzu kwa fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa taji hilo mwaka 1992, watakuwa wenyeji wa mechi ya kwanza ya fainali itakayochezwa kati ya Novemba 04 au 06.

Mechi ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye nchini Tunisia. "Jambo zuri kwetu ni kuanza mechi ya kwanza nchini Morocco," alisema beki huyo wa Ghana.

Esperance iliyolazimika kucheza Jumamosi iliyopita bila ya mashabiki wake walipocheza dhidi ya Al Hilal kutokana na kufungiwa wa Shirikisho la Soka Afrika kufutia vurugu za mashabiki wake.

Hata hivyo, mashabiki hao wataruhusiwa kushudia fainali wakati Esperance watakapokuwa na ndoto ya kurudia kile walichokifanya mwaka 1994 ili waweze kufuzu kwa Kombe la Dunia la Klabu la Fifa.

"Kila moja Ulaya atazama Ligi ya Mabingwa Afrika na sisi wachezaji tunakitu tunachokipata kutoka katika mashindano haya," alifafanua Afful.

"Kucheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Amerika Kusini katika Kombe la Dunia la Klabu ni kitu kizuri. Tunawatazama kila siku kwenye televisheni na kila wakati tunatama kucheza dhidi yao."

Kombe la Dunia la Klabu la Fifa mwaka 2011 linategemewa kufanyika nchini Japan kuanzia Desemba 08 hadi18.

Simba wazee wa dozi waendelea kutamba

















Ulimboka akijaribu kupiga majalo mbele ya beki wa Ruvu George Michael

Vinara wa ligi kuu na mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba jana waliendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu kwa kuichakaza Ruvu Shooting mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, huku watani zao Yanga wakishuka dimbani leo kuikabili Toto African.

Vinara hao walilazimika kusubili hadi kipindi cha pili kusherekea pointi tatu muhimu kwa vijana hao Msimbazi shukrani kwa mabao ya Emmanuel Okwi na Haruna Moshi aliyeingia akitokea benchi na kuifanya Simba kufikisha pointi 24.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji na kuhudhuriwa na watazamaji wachache kulinganisha na mechi zingine za Simba kwenye uwanja huo, ilikuwa na upinzani mkali tangu mwanzo mpaka mwisho.

Kiu ya kutaka kufunga mabao kwa Simba ilianza kwa shambulizi la dakika ya kwanza ya mchezo, baada ya washambuliaji wake Okwi, Felix Sunzu na Uhuru Seleman kugongea vizuri kabla ya jitihada zao kutibuliwa na mabeki wa Ruvu Shooting.

Ruvu Shooting inayoundwa na wachezaji chipukizi, ilijibu shambulizi hilo dakika saba baadaye, lakini kiki ya Abdallah Juma ilipaa juu ya lango, huku Jerry Santo wa Simba naye akikosa kwa staili hiyo ya kupaisha mpira juu ya mwamba dakika ya 18.

Vinara hao wa Ligi Kuu walitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, na nusura wabadilishe matokeo kama shuti la Uhuru lisingegonga mwamba na kurudi uwanjani kufuatia gonga nzuri na Sunzu.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Simba, Moses Basena ya kumtoa Uhuru na kumuingiza kiungo Haruna Moshi 'Boban' dakika ya 46, yalizaa matunda dakika moja baadaye kufuatia kazi nzuri ya Boban kumwezesha Okwi kufunga bao la kuongoza kirahisi kutokana na mabeki wa Ruvu kujichanganya.

Washambuliaji Simba waliojenga 'netiweki' nzuri ya ushambuliaji langoni mwa Ruvu baada ya kupewa 'dawa' ya kuongeza hamu ya kufunga mabao kama alivyodai kocha Basena, waliandika bao la pili safari hii likiwekwa kimiani na Boban.

Kocha wa Basena alisema wachezaji wake walicheza vizuri na kutegeneza nafasi nyingi za kufunga ni jambo la kujivunia kwa sababu uelewana wao umetoa ushindi.

Boban aliyeonekana kucheza vizuri na Okwi alifunga bao hilo kwa shuti kali dakika ya 54 na kumwacha kipa wa Ruvu, Benjamin Haule aliruka bila mafanikio.

Kocha wa Ruvu, Boniface Mkwasa alifanya madadiliko ya kuwatoa Abdallah Juma na Raphael Keyala na nafasi zao kuchukuliwa na Seif Abdallah na Abdallah Abraham.

Mabadiliko hayo yaliwapa nguvu Ruvu baada ya kufanya mashambulizi matano langoni mwa Simba katika muda mfupi, lakini yaliishia mikononi kwa kipa Juma Kaseja au kutibuliwa na mabeki wa Simba.

Ushindi huo umeifanya Simba kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo kwa kufikisha 24, baada ya michezo 10, huku ikiendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo mpaka sasa.

Mkwasa amesikitika kwa washambuliaji wake kutegeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia anajipanga kwa wakati ujao.
Wakati huo huo, ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mabingwa watetezi Yanga kuwavaa ndugu zao wa Toto African kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Toto mara ya mwisho walipokutana msimu uliopita mabingwa hao walishinda kwa mabao matatu.

Makocha wa pande zote mbili wameapa kuweka undugu pembeni na kuhaidi mchezo kusaka pointi tatu muhimu kwa kila mmoja.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya jana asubuhi kocha mkuu wa Yanga, Sam Timbe amesema anafahamu ubora na kiwango cha wapinzani wao na kikosi chake kipo kamili kukabiliana na wapinzani wao.

"Kila mmoja wetu anataka ushindi, nategemea upinzani mkubwa kwani timu ya Toto Afrikan ni nzuri na kila tukikutana nayo kunakuwa na upinzani mkubwa, wachezaji wote wako kwa sasa wako kwenye hali,"alisema Timbe.

Naye kocha wa Toto, John Tegete amesema historia si kigezo cha wao kupoteza kwani msimu huu wamejidhatiti kikamilifu kufuta uteja.
Tegete alisema kikosi chake kiko imara kukabiliana na mabingwa hao na anategemea mchezo kuwa mgumu kutokana na kila mmoja wao kuhitaji ushindi kwa namna yoyote.

Alisema wamecheza na Yanga mara nyingi na anatambua upinzani unaokuwepo mara timu hizo zinapokutana hivyo hana wasiwasi wowote kukabiliana na kikosi hicho huku akitamba wapo kamili kuivaa Yanga.

"Sitegemei mteremko wowote licha ya timu hizi kuwa karibu na sisi tupo ugenini kwa sababu huu ni ushindani na kila mmoja anataka apate nafasi ya kuwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo," alisema Tegete kwa akijiamini.

Yanga yenye pointi 15 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kiduchu dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopita huku wapinzani wao Toto wakiwa na pointi10 na kukamata nafasi ya tisa.