Wednesday, October 19, 2011

MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA 18 Oct 2011

Real Madrid ilipoichakaza Lyon 4-0

Manchester City Ilipoilipua Villareal 2-1

Bayern ilipotoa sare ya 1-1 na Napoli

Inter ilipoiadhibu Lille nyumbani kwao kwa 1-0


Wimbo wa leo, Aslay-Nakusemea

Msimamo Ligi kuu Uingereza

Msimamo wa Ligi Kuu ya England 

M TG PNT
1 Man City 8 21 22
2 Man Utd 8 19 20
3 Chelsea 8 11 19
4 Newcastle 8 5 16

5 Liverpool 8 2 14

6 Tottenham 7 1 13
7 Stoke 8 -2 12
8 Aston Villa 8 1 11
9 Norwich 8 -1 11
10 Arsenal 8 -5 10
11 QPR 8 -8 9
12 West Brom 8 -3 8
13 Swansea 8 -5 8
14 Fulham 8 1 7
15 Everton 7 -4 7
16 Wolves 8 -6 7
17 Sunderland 8 0 6

18 Bolton 8 -10 6
19 Wigan 8 -8 5
20 Blackburn 8 -9 5
 

Bondia David Haye atangaza kustaafu kuzichapa

David Haye, bondia wa Uingereza aliyekuwa bingwa wa zamani wa mkanda wa WBA, ametangaza kustaafu kutoka masumbwi.
Vladimir Klitschko na David Haye
Wladimir Klitschko na David Haye (kulia)
Haye, ambaye Alhamisi ametimia umri wa miaka 31, mara nyingi alinukuliwa akisema kwamba asingelipenda kupigana mara tu atakapotimia umri wa miaka 30.
Pambano la mwisho la Haye lilikuwa ni dhidi ya mpinzani Wladimir Klitschko wa Ukraine, tarehe 2 Julai, alipopoteza ubingwa wa mkanda wa WBA mjini Hamburg.
Awali kulikuwa na gumzo kuhusu matazamio ya Haye kurudi ulingoni na kupigana na Vitali, ambaye ni kakake Wladimir, mwaka 2012, licha ya habari za Jumanne kwamba bondia huyo wa London kamwe hakuwa na nia ya kuomba leseni mpya ya kuendelea na ndondi, leseni ambayo itakwisha mwezi Desemba.
Haye, ambaye alifanikiwa kusonga kutoka uzani wa cruiser hadi ule wa heavy, alipoteza ubingwa wake katika pambano la kujaribu kuwa bingwa wa kumiliki mikanda yote, baada ya kupigwa na Wladimir, ambaye alimshinda kwa pointi, na kutwaa ubingwa wa WBO, IBF na IBO.
Baadaye, Haye alidai alipigwa kutokana na maumivu ya kidole cha mguu ambacho kilikuwa kimevunjika.
Muingereza Haye alipata mkanda wa WBA baada ya kumshinda bondia wa Urusi, Nikolay Valuev kwa pointi nchini Ujerumani, mwezi Novemba, mwaka 2009.
Haye, ambaye alishindwa mara mbili tu katika mapambano 27 ya kulipwa, kisha aliweza kuutetea ubingwa wake kwa kumpiga Mmarekani John Ruiz katika ulingo wa mjini Manchester, Uingereza, mwezi Aprili, mwaka 2010.

Simba kuvaana na Ruvu Shooting leo

KOCHA wa wekundu wa msimbazi na vinara wa Ligi Kuu Bara-Simba, Moses Basena leo ana kipimo cha pili kuthibitisha ubora wa safu yake ya ushambuliaji aliyodai kuipatia 'dawa' ya kuongeza hamu ya kutia kambani, pale kikosi chake kitakapoivaa timu ngumu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Africa Lyon wiki iliyopita, ulikuwa wa kwanza mkubwa msimu huu kwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Basena anaamini kuwa kasi ya kufunga walioonyesha washambuliaji wake baada ya kuwapa maelekezo, leo itapata mwendelezo kama ilivyokuwa kwenye mechi dhidi ya Lyon.

Kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa naye amejipanga kuhakikisha timu yake inaitibulia Simba kwa kupanga jeshi la uhakika likiongozwa na wapachika mabao wake wake, Abdalah Juma, Revocatus Maliwa na Yusuph Mgwao kwa lengo ya kusaka mabao ya mapema.

Kwa upande wao Simba itaendelea kuwategemea washambuliaji wake Gervais Kago, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi watakaolishwa mipira na viungo Uhuru Selemani na Haruna Moshi 'Boban'.

Timu hizo zitashuka dimbani zikiwa zinatofautiana kwa pointi 10, kwani Simba inayoongoza ligi imejikusanyia pointi 21 mpaka sasa ikiwa imecheza michezo tisa wakati Ruvu Shooting inakamata nafasi ya saba ikiwa imejikusanyia pointi 11 huku ikiwa imeteremka dimbani mara tisa.

Simba ambayo ilirejea kwa kishindo katika uongozi wa ligi, ni dhahiri italazimika kufanya kazi ya ziada ili iweze kuibuka na ushindi hasa ukizingatia itaikabili Ruvu Shooting inayotumia mfumo wa soka la kasi na nguvu.

Akizungumzia pambano hilo, Basena alisema,"Kwanza kabisa tunatarajia kupata upinzani mkubwa ukizingatia sisi ndio tunaongoza ligi."

"Zaidi ya hapo nimewaambia wachezaji wangu wasahau matokeo ya ushindi wa mabao manne tuliyoyapata katika mechi yetu ya mwisho, wajue wana kazi ya kufanya ili tuendelee kushikilia nafasi tuliyopo, kwa mantiki hiyo nina imani tutashinda,"alisema Basena.

Naye Mkwasa alisema kuwa hawatarajii kupoteza mechi hiyo kwa mara nyingine na kuongeza kuwa vipigo walivyovipata msimu uliopita vinatosha na sasa ni zamu yao kutoa kipigo.

"Nimewaambia vijana wangu kwa nini kila siku watufunge?, ina maana hatujui mapungufu yetu au ni uzembe tu!, Simba ni timu nzuri sawa, lakini na sisi ni lazima tuonyeshe ni bora zaidi yao, vinginevyo itakuwa aibu,"alisema Mkwasa ambaye pia ni kocha wa timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars.

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni Sh 10,000 kwa jukwaa la viti maalumu (VIP) na Sh 5,000 kwa jukwaa la mzunguko.

BAADHI YA MECHI ZAWAHISHWA KUPISHA MECHI YA STARS NA CHADTaifa Stars inatarajia kuingia kambini Novemba 3 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayofanyika Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.

Ili kutoa fursa kwa wachezaji watakaoitwa Stars kuripoti kambini ndani ya muda uliopangwa, mechi za mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom zimefanyiwa marekebisho. Mechi hizo sasa zitachezwa Novemba 2 mwaka huu badala ya tarehe ya awali ya Novemba 5 mwaka huu.

Mechi hizo ni Oljoro vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid), Moro United vs Simba (Uwanja wa Taifa), Polisi Dodoma vs Yanga (Uwanja wa Jamhuri), Toto Africans v Azam (Uwanja wa CCM Kirumba), Kagera Sugar vs Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu) na Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi).

Kisa cha Muisraeli aliebadilishwa na wapalestina 1000



Tangu kutekwa kwake mapema Juni 25, 2006, Gilad Shalit aligeuka kuwa ndio turufu kubwa ya kundi la Hamas katika makabiliano yake na Israel.

Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 alivushwa hadi Gaza baada ya shambulio la Hamas. Israel iliapa kumkomboa bila ridhaa na kuanzisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Gaza.

Lakini hawakufanikiwa kumkomboa. Hamas siku zote ilikua na sharti moja tu - kwamba wafungwa takriban 1500 wa Kipalestinina waachiliwe kutoka jela - wengi wakiwemo waliohusika na mashambulizi mabaya ya mauaji dhidi ya raia wa kawaida.

Na akizungumza mwaka 2007 baba yake Gilad Noam Shalit alikiri kwamba hilo lingekuwa vigumu kwa Israeli kulikubali.

Juhudi za upatanishi ziliongozwa na maafisa wa Ujerumani na Misri.

Masharti ya kimsingi yakabainika wazi na hayatofautiani na mpango huu unaotekelezwa sasa wa kubadilishana wafungwa. Lakini juhudi hizi hazikufua dafu.

Na sababu moja ilikua waziri mkuu wa Israel wakati huo Ehud Olmert alikuwa dhaifu kisiasa hadi kwamba hakuwa na ubavu wa kulazimisha makubaliano.

Lakini kampeni ya kushinikiza Gilad aachiliwe huru ikiongozwa na wazazi wake ilizidi kupata msukumo.

Mapema mwaka 2009 Israeli ilianzisha mashambulio makubwa katika Gaza kwa lengo la kumkomboa Gilad Shalit lakini haikufanikiwa.

Baadae makubaliano yalifikiwa kwa kuachiliwa wafungwa 20 wanawake wa Kipalestina kwa kubadilishana na video ya Gilad ambayo ilithibitisha kuwa yuko hai.

Gilad alionekana amekonda sana ingawa alikuwa na hali nzuri ya afya.

Picha hizo zilisaidia kumfanya awe nembo kubwa zaidi nchini Israel ambayo siku zote imefanya juhudi kubwa za kuhakikisha kwamba inawarudisha wanajeshi wake waliotekwa, hata kama wamerejea maiti.

Lakini msemaji wa waziri mkuu mpya , Benjamin Netanyahu, bado hakutaka kufikiria wazo lolote la kutoa ridhaa kwa kundi la Hamas.

Familia ya Gilad iliimarisha kampeni yake ya kufikiwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa wakiungwa mkono na vyombo vya habari vya Israeli na kuendeleza shinikizo kwa kuandamana kutoka nyumbani kwao hadi makao ya Bw Netanyahu.

Hamas nayo haikuonyesha ishara yoyote ya kubadili msimamo wake.

Hatimae ni wazi kabisa kwamba kitu kilichoshawishi serikali ya Israeli na Hamas kwamba makubaliano yangezinufaisha pande zote mbili ni mageuzi makubwa ya kisiasa yaliyotokea Mashariki ya kati mwaka huu.

Pande zote mbili zilikabiliwa na changamoto mpya na zilihitaji angalau kwa sasa kuimarisha umaarufu wao ambao wangeupata kwa kubadilishana wafungwa.

MUISRAELI 1 ANA THAMANI YA WAPALESTINA 1000

Makundi ya watu wenye furaha nchini Israel na Palestina wamekuwa wakisheherekea mpango wa kihistoria wa kubadilishana wafungwa.

Israel iliwaachiliwa huru mamia ya wafungwa wa Kipalestina, ikiruhusu wengi wao kurudi katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, na badala yake kukabidhiwa askari wa Kiisrael Gilad Shalit.

Sajini Shalit aliyekuwa amezuiliwa katika eneo la Gaza kwa zaidi ya miaka mitano, alipokelewa kishujaa alipowasili nyumbani kwake.

Shalit mwenye umri wa miaka 25, hatimaye alilala nyumbani kwao na familia yake kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa huru.

Babake Shalit amesema mwanawe ana matatizo ya kutangamana na watu kutokana na kuzuiliwa kifungo cha upweke cha miaka mingi, kwa hivyo hangeweza kuhutubia waliojitokeza kumkaribisha.

Alisema anaeleewa machungu yanayozikumba familia ambazo zimepoteza wapendwa wao waliouawa na Wapalestina walioachiliwa huru wakati wa kubadilishana wafungwa.
Ghilad Shalit awasili Israel
Waziri wa ulinzi,waziri mkuu Netanyahu na baba yake Ghilad Shalit wakimkaribisha Shilat

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wa viongozi wa kundi la kiislamu la Hamas walioafikiana kuhusu kubadilishanaji kwa wafungwa hao, walisifu hatua hiyo kama thibitisho la sera zao.

Lakini waandishi wa habari wamesema kubadilishana kwa wafungwa huenda kusiwe na athari kubwa katika mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.

Wakati hayo yakijiri, zaidi ya watu laki moja walijumuika katika ukumbi maalum mjini Gaza kusherehekea kuachiliwa huru kwa nusu ya zaidi ya Wapalestina 1000.

Mji wa gaza uko chini ya kundi la Hamas na kiongozi wa kundi hilo Khaled Meshal alisema limepata ushindi mkubwa kufuatia hatua hiyo.