Friday, August 26, 2011

Mwanadada Eva Carneiro daktari mpya wa Chelsea



Eva Carneiro akiwa katika benchi la Chelsea



Drogba akikatiza katika Benchi la Chelsea kushoto anaonekana Daktari wa timu mwanadada Eva, sasa sijui Drogba ndio anauza sura kwa kujipitisha ili aopoe?



Benchi la wachezaji wa akiba la Chelsea kushoto kocha Ferreira na kushoto mwisho mwanadada daktari Eva Carneiro

Tetesi za usajili Majuu zilizotoka hivi punde

Juventus yamuwania Malouda
Mkurugenzi wa Juventus Giussepe Marota ameeleza waziwazi juu ya kumhitaji Malouda katika kikosi chake, kama wakikubaliana watamchukua Malouda mwenye miaka 31 kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 5.

Alvaro Perreira kutua Chelsea
Wakati wanatarajia kumuuza Malouda Chelsea wametangaza kuongeza dau kumnasa mchezaji wa Porto ambaye ni raia wa Uruguay Alvaro Perreira, baada ya Porto hapo awali kukataa kitita cha paundi za uingereza milioni 16.6 na sasa wapo tayari kuongeza dau kumnasa Perreira.

Emanuele Giacherini atua Juventus
Juventus imefanikiwa kumnyaka Emanuelle 26, kutoka klabu ya Cesena na hivi sasa yupo Turin akifanyiwa vipimo vya afya.

LEONEL MESSI MCHEZAJI BORA ULAYA 2011-2012 Xavi namba 2, Ronaldo aambulia kura 2

Lionel Messi
MESSI

Leonel Messi mshambuliaji wa kutisha na kuogopwa wa F.C Barcelona ya Spain ameibuka kidedea na kuwa mchezaji bora zaidi wa soka barani ulaya 2011-2012.
Messi alitangazwa mshindi baada ya droo iliyofanyika Monaco kupanga makundi ya klabu bingwa ulaya 2011-2012, katika kinyang'anyiro hiko Messi aliwapiku Xavi kwa kura 11 na kuwa wa pili huku akimzidi Christian Ronaldo wa Real Madrid aliyekuwa wa tatu kwa kura nyingi ambapo Ronaldo aliambulia kura tatu tu.

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

1 Lionel Messi (ARG) – FC Barcelona (39 votes)
2 Xavi Hernández (ESP) – FC Barcelona (11 votes)
3 Cristiano Ronaldo (POR) – Real Madrid CF (3 votes)
4 Andrés Iniesta (ESP) – FC Barcelona
5 Falcao (COL) – ex FC Porto (Club Atlético de Madrid)
6 Wayne Rooney (ENG) – Manchester United FC
7 Nemanja Vidić (SRB) – Manchester United FC
8 Zlatan Ibrahimović (SWE) – AC Milan
Gerard Piqué (ESP) – FC Barcelona
10 Manuel Neuer (GER) – ex FC Schalke 04 (FC Bayern München)

Fainali UEFA Super Cup ni BARCELONA vs F.C PORTO leo

 FC Barcelona vs FC Porto
Leonel Messi mchezaji bora wa ulaya 2011-2012

Fainali ya UEFA super Cup Leo inawakutanisha wababe wawili yaani Barcelona ya Spain na F.C Porto. Mchezo huo utakaopigwa leo 26 agosti 2011 majira ya saa 18:45-20:45 GMT katika dimba la Stade Louis II jijini Monaco.
Barcelona bingwa mtetezi wa kombe hilo anakutana na bingwa wa ligi ya ulaya F.C Porto, Barcelona imeshachukua kombe hilo mara 3 wakati F.C Porto wamelinyaka mara 1 tu, Barcelona ni ya 2 kwa ubora ulaya 2011-2012 na F.C Porto ni ya 7 kwa takwimu za Shirikisho la soka la ulaya(UEFA).

Katika mechi hiyo timu zinatarajiwa kupangwa kama ifuatavyo;

FC Barcelona :
David Villa, Lionel Messi, Victor Valdes, Adriano Correia, Daniel Alves; Sergio Busquets, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Eric Abidal, Javier Mascherano, Pedro Rodriguez.


FC Porto :
Helton,Fucile, Souza, Joao Mourinho, Freddy Guarin, Alvaro Pereira, Rolando, Otamendi, Varela/James Rodriguez, Kleber, Hulk.

MAKUNDI KLABU BINGWA ULAYA MAN CITY KUNDI LA KIFO, ARSENAL USO KWA USO NA MARSEILLE, MAN UNITED NA BENFICA, CHELSEA NA VALENCIA



Katika droo iliyochezeshwa jana kupanga timu katika hatua ya makundi Timu ya Man City ndio inatajwa kuwa katika kundi la kifo ikikutana na Bayern Munich ya Ujeruman,Villareal ya Spain na Napoli ya Italia. Makundi yako kama ifuatavyo;

Group A:
Bayern Munich, Villarreal, Manchester City, Napoli.

Group B:
Inter Milan, CSKA Moscow, Lille, Trabzonspor.

Group C:
Manchester United, Benfica, Basle, Otelul Galati.

Group D:
Real Madrid, Lyon, Ajax, Dinamo Zagreb.

Group E:
Chelsea, Valencia, Bayer Leverkusen, Genk.

Group F:
Arsenal, Marseille, Olympiakos, Borussia Dortmund.

Group G:
FC Porto, Shakhtar Donetsk, Zenit St Petersburg, Apoel.

Group H:
Barcelona, Ac Milan, Bate Borisov, Viktoria Plzen

KIKOSI STARS CHATANGAZWA COSTA NDANI CANNAVARO OUT

Sosthenes Nyoni
BAADA ya takribani miaka minne, hatimaye beki wa kimataifa wa Tanzania na Simba,Victor Costa ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, huku Nadir Haroub akiachwa kwa mara ya kwanza tangu 2006.

Kocha Jan Poulsen jana alitangaza kikosi chake cha wachezaji 22 kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Algeria hapo Septemba.

Akitangaza kikosi hicho jana kwa Wanahabari jijini Dar es Salaam, Poulsen kwa mara ya kwanza tangu alipokabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi hicho amemwacha beki kisiki wa timu hiyo na Yanga, Haroub 'Canavaro' sambamba na kumrejesha kipa Juma Kaseja wa Simba.

Poulsen ambaye katika kikosi chake alichokiita kwa ajili ya mechi dhidi Sudan aliwaengua wachezaji wote, lakini jana aliwajumuisha wachezaji hao wa kulipwa Tanzania wanaocheza nje ya nchi.

Wachezaji hao sita wanaocheza soka ya kulipwa nje ya nchi ni Mbwana Samata (TP Mazembe, DRCongo) akiwamo Henry Joseph (Kosvinger, Norway), Nizar Khalfan (Whitecaps, Canada), Abdi Kasim 'Babi' na Dany Mrwanda (Long, Vietnam) na Athuman Machupa (Vasslander, Sweden).
Beki Costa ambaye hivi karibuni alirejea katika kikosi cha Simba akitokea klabu ya HCB Songo ya Msumbiji, mara ya mwisho aliichezea Taifa Stars kwenye mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika 2008 dhidi ya Msumbiji mwaka 2007, wakati huo Stars ikiwa chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo.

Poulsen alisema sababu iliyomsababisha kumwita Costa licha ya kumwona katika mechi moja tu ya Simba dhidi Yanga alisema alizingatia ushauri aliopewa na baadhi ya makocha wenzake waliomweleza kwamba mchezaji huyo ni mmoja kati ya mabeki bora nchini.

Poulsen akizunguzia pambano dhidi ya Algeria na nafasi ya Stars kufuzu kwa fainali hizo alisema Algeria ni kati ya timu imara Afrika, ikumbukwe kwamba mara kadhaa imebadili kocha kwa lengo la kuhakikisha wanafanya vizuri, kufungwa mabao 4 na Morocco haimaanishi wao ni legelege.

"Wakati mwingine ni vizuri tukawa wakweli na wawazi, nafasi yetu ya kufuzu ni finyu sana na hii ni kutokana na matokeo ya kundi letu lilivyo, lakini sisemi kwamba hatutakiwi kupambana hapana, tunaichukulia mechi hii kwa umuhimu mkubwa kwa vile pia itakuwa sehemu ya kujiweka sawa kabla ya kucheza na Chad mwezi Novemba."

Katika hatua nyingine Poulsen alilalamikia nidhamu mbovu kwa wachezaji uwanjani na kukosa moyo wa kujituma ndiyo sababu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kutofanya vizuri katika medani ya soka ulimwenguni ukilinganisha na nchi ya Ulaya.

"Mimi hapa nimeshawaita mara kadhaa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi, lakini utakuta hawaji wote, Abdi Kasim alifunga bao kule Algeria, lakini tangu hapo haji kuichezea nchi yake tena hivyo hivyo kwa Samata tulipocheza na Afrika Kusini hakuonekana, hili ni tatizo kubwa kwa Tanzania na Afrika," alisema Poulsen.

Kikosi kamili cha Poulsen ambacho kitakachoingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa ni pamoja na makipa, Shaaban Dihile, Juma Kaseja na Shabani Kado, wakati mabeki wa pembeni ni Shadrack Nsajigwa, Idrisa Rajabu na Amir Maftah.
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris, Juma Nyoso na Victor Costa, viungo ni Henry Joseph, Nurdin Bakar, Shaaban Nditi, Juma Seif 'Kijiko' na Jabir Aziz, Nizar Khalfan, Mrisho Ngasa na Salum Machaku.
Washambuliaji ni pamoja na Mbwana Samata, Abdi Kassim, 'Ramadhan Chombo, John Boko na Athuman Machupa.