Thursday, August 18, 2011

TAZAMA VIDEO JINSI BARCA ILIVYOICHARAZA REAL MADRID


Iniesta akitia nyavuni bao la kwanza




Messi akitia kwenye kamba goli la pili


Benzema akiisawazishia Real goli la pili


Ronaldo akipachika bao la kwanza kwa Real Madrid


Marcello amchezea vibaya Fabregas



SIMBA YAILIZA YANGA 2 KWA BUYU

Sunzu akishangilia baada ya kutia kambani goli la pili

SIMBA, Simba ndio ulikuwa wimbo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada vijana hao wa mtaa wa Msimbazi kulipinza kisasi kwa ukifunga Yanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Simba waliofungwa kwenye Kombe la Kagame na Ngao ya Jamii mwaka jana vijana hao wa Mganda Moses Basena walizinduka na kupata mabao ya mapema kupitia kiungo Haruna Moshi 'Boban' dakika 15 na penalti ya Felix Sunzu dakika 38.

Simba iliyoanza kwa kasi mchezo huo ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Moshi 'Boban' aliyemalizia vizuri krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Sunzu aliyekuwa na ushirikiano mkubwa na Emmanuel Okwi.

Mshambuliaji Sunzu alifungia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Nadir Haroub kumchezea vibaya Moshi 'Boban', kwenye eneo la hatari dakika 35. Sunzu alilazimika kuonyesha ueledi wake pale alipotakiwa kurudia penalti hiyo baada ya mwamuzi Israel Mjuni kusema Kado alitokea kabla ya kupigwa kwa penalti ya kwanza pamoja na kuwa alikuwa amefunga.

Kocha Moses Basena aliyeonekana kujifunza kwa makosa alitumia mfumo wa 4:2:3:1 na kutoa nafasi kubwa kwa Okwi, Haruna na Sunzu kutawala sehemu kubwa ya kiungo tofauti na ilivyokuwa kwenye fainali ya Kombe la Kagame.

Okwi alifanya atakalo mbele ya mabeki wa Yanga walionekana kuwa kama watu waliozidiwa na mazoezi na kukosa unyumbulifu mchezoni, huku safu ya ulinzi wa Simba chini ya mkongwe Victor Costa aliweza kuwapoteza mchezoni kabisa mshambuliaji Keneth Asamoah na Jerry Tegete.

Kiungo Haruna Niyonzima alijitahidi kuonyesha uwezo mkubwa wa kutawala mpira na kujaribu kutafuta goli kwenye mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi, lakini alikosa msahada kutoka kwa wenzake.

Simba ilianza mashambulizi kwa kasi na dakika kwanza Okwi alikosa bao baada ya shuti lake kumgonga Haroub na kupaa juu ya goli.

Okwi alipoteza nafasi nyingine dakika 8 baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Yanga, lakini aliugonga mpira mbele zaidi na kipa Shaaban Kado akauwahi.

Beki wa Yanga, Chacha Marwa, nahodha Shadrack Nsajigwa alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Okwi. Naye Juma Nyoso wa Simba alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Asamoah.

Haruna Niyonzima alipiga shuti la umbali wa mita 25 baada ya kumchungulia Juma Kaseja kwa bahati mpira huo ulipaa juu ya goli.

Kipindi cha pili Yanga iliamka baada ya kuingia Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo lakini walishindwa kuipenya ngome ya Simba.

Yanga waliendeleza sera yao ya kugomea jezi za wadhamini wa ligi Vodacom zenye nembo nyekundu kwa kuvaaa jezi za mdhamini wao TBL tofauti na Simba wenyewe walivaa zile walizopewa na Vodacom

Vikosi Yanga;
Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Chacha Marwa, Juma Seif, Godfey Taita, Haruna Niyonzima, Keneth Asamoah/ Gumbo, Jerry Tegete, Kigi Makasi/ Kiiza.
Simba: Juma Kaseja, Said Nasoro, Amir Maftah, Juma Nyoso, Victor Costa, Partick Mafisango, Salum Machaku/ Kiemba, Jerry Santo, Felix Sunzu, Haruna Moshi/ Gervais Kago, Emmanuel Okwi/ Kapombe

UFISADI INDIA MARUFUKU WANANCHI WAANDAMANA

Maelfu ya raia India wamejitokeza mitaani kumunga mkono mwanaharakati wa kupinga ufisadi Anna Hazare.
manmohan singh na anna hazare
Maelfu ya watu nchini India wamekerwa na viwango vya ufisadi
Awali wafuasi wa Bw Hazare walikusanyika nje ya jela mmoja mjini Delhi ambako amekuwa akizuiliwa tangu jumanne.
Bw Hazare amegoma kuondoka katika jela hilo hadi serikali ya India itakapo mruhusu kutekeleza mpango wake kususia kula chakula hadharani.
Mwanaharakati huyo anahurumiwa na wengi nchini India na tayari maandamano ya kumuunga mkono yanazidi kuvutia idadi kubwa ya watu kote nchini humo.
Bw Hazare anashinikiza kufanyika kwa mageuzi katika sheria za kupambana na rushwa na alikuwa amepanga kuanza kukesha bila chakula ili kushinikiza hilo lifanyike.
Watu wengi wanaomuunga mkono wamejitokeza na mabango huku wakikemea serikali wakitaka aachiwe huru.
Raia hao wa India wanasema lazima serikali ichukue hatua za kukabili ufisadi uliokithiri nchini humo.
Hata hivyo waziri mkuu wa India Manmohan Singh amemkosoa mwanaharakati huyo akisema, ingawa nia yake ni nzuri anatumia dhana potufu kulazimisha bunge lifuate matakwa yake.
Mshirika wa karibu wa Bw Hazare amesema kuwa sasa amekubali kuondoka jela baada ya polisi kuridhia kuwa anaweza kufanya mgomo huo wa kususia chakula kwa siku kumi na tano kwenye bustani mmoja mjini Delhi.
Bw Hazare na wafuasi wake 1,200 walitiwa nguvuni na polisi wakiwa kwenye bustani ya JP park saa chache kabla waanza kusisia chakula.
Mwezi April, Bw Hazare alivunja mgomo wake wa kususia chakula baada ya siku nne pale serikali ilikubali kuwa anaweza kuhusika kuandaa mswada wa kupambana na ufisadi nchini humo ambapo kutakuwa ofisi maalum ya kuchunguza wanasiasa na watumishi wa serikali wanashukiwa kuhusika na ufisadi.
Mwanaharakati huyo mwenye miaka 74, hata hivyo anapinga mswada uliowasilishwa bungeni kwa kuwa waziri mkuu na majaji hawata chunguzwa.