Friday, July 8, 2011

SIMBA DUME LA MBEGU LATINGA FAINALI KAGAME

Kikosi cha timu timu ya Simba
Timu ya Simba Sports Club ama wekundu wa msimbazi kama wanavyojulikana wametinga fainali katika michuano ya kagame baada ya kuiondosha timu ngumu ya El-Mereikh ya Sudan kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoshana nguvu ya bao moja kwa moja ndani ya dakika 90,na badae kuongezwa dakika 30 lakini mambo yakabaki vilevile ndipo ilipoamriwa kupigwa mikwaju ya penati.Katika mikwaju ya penati Simba walimalizia mkwaju wa mwisho na wa ushindi ukipigwa na mafisango na El Mereikh walipokosa mkwaju wa mwisho katika penati ya sita Wekundu wa msimbazi waliamka vitini kwa nderemo na vifijo wakiwa tayari wametinga fainali,shujaa katika mchezo huo alikuwa ni golikipa namba moja tanzania Juma Kaseja baada ya kuokoa mkwaju wa penati na kuiwezesha kutinga fainali.

Umati wa mashabiki wa Simba wakishangilia katika mechi hiyo.
Wekundu hao inawabidi kusubiri mshindi wa leo katika nusu fainali nyingine kati ya wapinzani wao wa jadi Dar Young Afrikans (Yanga) dhidi ya St George ya Ethiopia katika mchezo utakaounguruma katika dimba kuu la taifa jijini Dar Es Salaam.

Shujaa katika mechi hiyo golikipa Juma Kaseja