Friday, June 24, 2011

HOMA YA MPAMBANO DAVID HAYE vs WLADIMIR KLITSCHKO

Mpambano wa masumbwi ya uzito wa juu kati ya Wladimir Klitscho dhidi ya bingwa mtetezi David Haye imezidi kupamba moto huku kila mmoja yeye pamoja na mashabiki wake wakijigamba kufanya vyema katika mpambano huo unaotarajiwa kufanyika julai 2, 2011 katika ukumbi wa Imtech Arena jijini Hamburg nchini Ujerumani. Mpambano huo utakuwa wa uzito wa juu kabisa ukijulikana kama "HEAVYWEIGHT" utakuwa wa kuwania mataji matatu ambayo ni mkanda wa chama cha ngumi ulimwenguni,mkanda wa shirikisho la ngumi za kimataifa na mkanda wa shirika la ngumi ulimwenguni. David Haye ndie ambaye anashikilia ubingwa huo kwasasa. Na ifuatayo ni taarifa fupi kuhusu Wanamasumbwi hawa.

David Haye


Dokezo muhumu kuhusu David Haye,
  • Nickname:Hayemaker

  • Rated at: Heavyweight

  • Height: 191cm (6ft 3in)

  • Nationality: British

  • Birth Date: 13/10/1980 (age 30)

  • Birth Place: London, Eng

  • Stance: Orthodox

  • Record

    • Fights: 26
    • Wins: 25
    • KOs: 23
    • Draws: 0
    • Losses: 1
    • Mechi sita za mwisho.

      • 13/11/10: Audley Harrison W TKO3
      • 03/04/10: John Ruiz W TKO9
      • 07/11/09: Nikoali Valuev W PTS
      • 15/11/08: Monte Barrett W TKO5
      • 08/03/08: Enzo Maccarinelli W TKO2
      • 10/11/07: Jean-Marc Mormeck W TKO7


    Wladimir Klitschko

    Dokezo muhimu kuhusu Wladimir Klitschko,

      Nickname:Dr Steelhammer
  • Rated at: Heavyweight

  • Height: 199cm (6ft 6½in)

  • Nationality: Ukrainian

  • Birth Date: 03/25/1976 (age 35)

  • Birth Place: Semipalatinsk, Kaz

  • Stance: Orthodox

  • Record

    • Fights: 58
    • Wins: 55
    • KOs: 49
    • Draws: 0
    • Losses: 3
    • Mechi sita za mwisho.

        • 11/09/10: Samuel Peter W KO10
        • 20/03/10: Eddie Chambers W KO12
        • 20/06/09: Ruslan Chagaev W RTD9
        • 13/12/08: Hasim Rahman W TKO7
        • 12/07/08: Tony Thompson W KO11
        • 23/02/07: Sultan Ibragimov W PTS

    CLICHY ANATAKA KWENDA LIVERPOOL

    Gael Clichy
    Beki wa Arsenal Gael Clichy binafsi amesema anahitaji kwenda Liverpool. Akiwa amebakiza miezi 12 mkataba wake na Arsenal uishe mchezaji huyo anataka kuishawishi Asenal kufanya mazungumzo na Liverpool ambayo imetoa ofa ya paundi za Uingereza milioni 5, Maamuzi hayo ni ya kushangaza kidogo kwani tayari klabu ya AS Roma ya Italy tayari imeshatangaza dau la paundi za Uingereza milioni 7 ikiwa ni milioni 2 zaidi ya dau la Liverpool lakini Clichy inaonekana anafurahia zaidi kuendelea kubaki Uingereza.

    MANUEL JURADO ATAJWA KUMRITHI CSEC FABREGAS.

    Klabu ya AS Roma ya Italy ipo katika mpango wa kumnasa chipukizi wa Barcelona Bojan Krkic kwa kitita cha euro milioni 10. Hii ina maana kwa Barcelona kuweza kutumia pesa hizo na kuongeza zingine ili kumnasa Kiungo wa Arsenal Csec Fabregas. Wenger ili kujiandaa na maisha bila ya Fabregas tayari ameshaweka malengo ya kumnasa kiungo mchezeshaji wa Schalke 04 Juan Manuel Jurado, ambapo mpango wa Wenger ni kutumia paundi za Uingereza milioni 7.5, Jurado aling'ara zaidi katika fainali za ligi ya mabingwa ulaya 2010-2011 ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliiwezesha Schalke 04 kufika nusu fainali.

    WENGER AJIPANGA KUMNASA DIARRA

    Mahamadou Diarra
    Meneja wa timu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger anajipanga kumnasa nyota wa Real Madrid Mahamadou Diarra. Habari zinasema Wenger anajipanga kumpa Diarra mkataba wa mwaka mmoja na kumtengea mshahara wa paundi za Uingereza 50,000 kwa wiki.

    MELLO ACHUKIZWA KUBADILISHWA NA MEIRELES

    Felipe Mello

    Raul Meireles
    Kiungo wa Juventus Fellipe Mello amekasirishwa na hafurahii kitendo cha cha uongozi wa Juventus kumtoa "kafara" na pesa kidogo ili kumnasa mchezaji wa Timu ya Liverpool mreno Raul Meireles. Juventus wapo tayari kumtoa Mello na kitita cha paundi za Uingereza milioni 13 ili kumnasa Meireles.Akiwa hajatimiza hata mwaka tangu asajiliwe na Liverpool akitokea Porto kwa ada ya paundi za Uingereza milioni 10,Meireles sasa anahitajiwa na Juventus kwa udi na uvumba. "Kwa hiyo tuseme Juve hawaniheshimu,hicho ndio nachoweza kusema" Mello aliliambia gazeti la Daily Mirror, "Yaani mi si lolote?,mi sio wa kujadiliana kwa bei nafuu" aliongeza Mello.

    BARCELONA WATAJA DAU KUMNG'OA FABREGAS.

    Csec Fabregas
    Habari ya kweli ambayo imeripotiwa na magazeti mengi ya leo asubuhi ni kwamba Timu ya Barcelona ya Uhispania imetaja kuwa inataka kumsajili kiungo wa Arsenal ya Uingereza Csec Fabregas kwa kitita cha Paundi za Uingereza milioni 27.