Saturday, June 18, 2011

PICHA YA LEO

WACHEZAJI GHALI NA WANAOLIPWA ZAIDI 2011.

Unaweza kuwaita kuwa ndio wachezaji ghali na matajiri,vilevile ukawaita ndio wachezaji bora zaidi duniani. Kwa hivi sasa wachezaji ghali zaidi ni kama ifuatavyo;

1} CHRISTIAN RONALDO, Huyu ndiye mchezaji ghali zaidi aliyegharimu uhamisho wa paundi za uingereza milioni 80, kutoka Man U kwenda Real Madrid. Huu ndio uhamisho ghali zaidi kuwahi kutokea katika soka ambao mpaka sasa bado ni gumzo.

2} RICARDO KAKA, Huyu anasadikika kuwa ndiye mchezaji bora na mwenye kasi aliyewahi kutokea katika ulimwengu wa soka. Ambapo aliigharimu Real Madrid kitita cha Paundi za uingereza milioni 56 kumng'oa katika kikosi cha AC Milan ya Italy. Pamoja na kuwa na kipaji na ujuzi, Kaka hakuweza kuonesha makeke yake akiwa Real kutokana na kuwa majeruhi mara kwa mara lakini hamna shaka anaweza kurudi katika kiwango chake pale atakaporejea katika hali yake.
3} ZLATAN IBRAHIMOVIC, Huyu alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani,na alikuwa katika kiwango cha hali ya juu katika kipindi cha mwaka 2007-2008 katika msimu wa ligi ya Italy. Alinyakuliwa na Barcelona kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 60.7 kutoka Inter Milan ya Italy.

4} FERNANDO TORRES, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji bora katika ligi ya Uingereza ambapo mwaka 2007-2008 alishika nafasi ya pili kama mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza namba moja akiwa ni Christian Ronaldo. Torres alinyakuliwa na Chelsea ya Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 50 kutoka Liverpool pia ya Uingereza. Pamoja na kutokufanya vizuri akiwa Chelsea Torres bado ananafasi ya kufanya vizuri akiwa na Chelsea katika msimu ujao wa ligi.
5} ZINEDINE ZIDANE, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji wenye ujuzi "skillfull" duniani, amliichezea Ufaransa mara mbili katika kombe la dunia na kuiwezesha Ufaransa kutinga fainali mwaka 2006.

6} LUIS FIGO, Huyu alikuwa ni ni mchezaji mzuri sana na inaaminika katika kipindi chake alikuwa mchezaji bora duniani ambapo aliigharimu Barcelona kumng'oa kutoka Real Madrid kwa paundi za Uingereza milioni 37.

7} HERNAN CRESPO, Crespo alikuwa ni mchezaji wa hali ya juu kipindi Figo yupo kwenye chati,na inaaminika Crespo ni kati ya wachezaji bora duniani ambapo alinunuliwa kwa paundu za Uingereza milioni 35.5 na timu ya Lazio ya Italy akitokea Parma pia ya Italy.

8} ANDY CAROLL, Huyu alipata uhamisho sio siku nyingi sana ni 2011 kutoka Newcastle kwenda Liverpool zote za Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35.
9} DAVID VILLA, Huyu hivi sasa ndio yupo katika kiwango chake,alipata kiatu cha dhahabu na akiwa ni miongoni wa wafungaji bora katika fainali z kombe la dunia 2010 akiichezea Uhispania. Alinyakuliwa na Barcelona Uhispania kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 34.2 akitokea Valencia pia ya Uhispania. Villa anategemewa kufanya mazuri zaidi kama atabaki Barcelona.
10} GIANLUIGI BUFFON, Ukiongelea golokipa bora katika historia ya soka....Buffon anasadikika kuwa golikipa bora zaidi duniani baada ya Oliver Kahn wa Ujerumani. Huwa haijalishi ni timu gani anachezea ana uwezo wa kupangua michomo ambayo huwafanya wachezaji wenzake warudi mchezoni, alisajiliwa na Juventus kwa paundi za Uingereza milioni 32.6 akitokea Parma zote za Italy. Buffon amemuoa mwanamitindo wa Czeck Seredova.