Tuesday, June 14, 2011

PICHA YA LEO

Upendo ni kitu muhimu sana katika maisha ya kiumbe chochote chini ya jua.

TOFAUTI YA PROFILE ZA WASICHANA/WANAWAKE NA WAVULANA/WANAUME KATIKA FACEBOOK

Mtandao wa kijamii wa Facebook maarufu kama FB umezidi kuchukua umaarufu siku hadi siku na katika hilo naweza kusema mtandao huu wa kijamii umeteka Dunia.
Katika mtandao huu watu hupata marafiki aidha kwa kujuana au kwa kujuana ki facebook facebook tu na kuombana urafiki kisha wanaendelea na mawasiliano. Kuna kitu kinaitwa Profile hapa ni pale ambapo habari binafsi za mwanachama hupatikana kama vile yeye ni nani,yupo wapi na anafanya shughuli gani vilevile unapata kuona picha zake ambazo amezihifadhi yeye.
Katika hizi PROFILE nimegundua kuwa za wasichana au wanawake zipo tofauti sana na za wale wa jinsia ya pili yaani wanaume, Tofauti hiyo ni hii;
Mwanamke akiandika kitu katika sehemu ya status kwa mfano; Najisikia vibaya......
Mwanaume nae aandike mfano; nimepata ajali nimeumia sana......
Sasa basi status ya mwanamke ina dakika moja tu tangu aandike, na mwanaume ina siku nne tokea aiandike lakini matokeo yatasomeka hivi;
Katika muda huo mfupi mwanamke atakuwa na likes 60, mwanaume atapata likes 1.
watakao comment kwa mwanamke watafikia 104 wakati mwanaume atapata comment 3.
Ukisoma walicho-comment kwa mwanamke kitasomeka hivi, Imekuwaje?
Sasa ninajiuliza mwanamke kaandika tu..najisikia vibaya lakini mwanaume kaandika kitu serious kwamba amepata ajali lakini duh..kila mtu anahitaji kuwasiliana na mwanamke,haya ndio yanayotokea katika mitandao mingi ya kijamii hasa FACEBOOK.

HAKUNA MBINU MBADALA KUKABILIANA NA GHASIA ZAIDI YA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO?

Maandamano na migomo ni haki za msingi kwa mwananchi yeyote yule ili mradi maandamano hayo au mgomo huo ufuate kanuni na taratibu na vyote hivyo vifanyike pasipo kukiuka au kuvunja sheria na kanuni za nchi. Sasa basi bila kujali kuwa maandamano au mgomo umefuata taratibu au la, nijuavyo mimi maandamano au migomo huwa ni katika kutafuta haki ambayo kwa namna moja au nyingine imenyimwa au imenyang'anywa iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi na ili ipatikane lazima kuwe na shinikizo la amani yaani maandamano au mgomo.
Hali imekuwa mbaya sana pindi migomo au maandamano yanapotokea iwe kwa kufuata taratibu au kwa kutifuata taratibu,waandamanaji huwa hawana nia ya kudhuru zaidi ya kutaka kusikilizwa, lakini cha kushangaza jeshi letu la polisi limeonesha udhaifu kwani mara kwa mara hupenda kutumia silaha za moto katika kukabiliana na waandamanaji kitu ambacho si sahihi kwasababu waandamanaji huwa hawana silaha sasa iweje polisi watumie silaha kukabiliana nao? Hili linanipa wasiwasi kwamba jeshi letu la polisi limekosa ubunifu na halina ujuzi wowote wa kukabiliana na waandamanaji na wanaona suluhisho ni kurusha silaha za moto ambazop matokeo yake zimekuwa zikiua na kujeruhi wananchi ambao kwa namna moja au nyingine huwa hawana makosa.
Wakati mwingine huwa inanipa hisia mbaya na kufikiria kuwa hawa askari wetu pindi zinapotokea purukushani basi wao huona hapo ndio pa kuonesha utaalamu wao wa kufyatua risasi kwa hali halisi askari anaweza akaanza kazi mpaka akastaafu bila kufyatua risasi zaidi ya kwenye mafunzo.
Ushauri wangu kwa jeshi letu ambalo ndilo lenye dhamana ya kusimamia usalama wetu na mali zetu wajipange upya katika kukabiliana na migomo au maandamano pasipo kudhuru wananchi kwani hili linaleta chuki kati ya jeshi la polisi na wananchi, siamini kuwa hakuna njia nyingine ya kukabiliana na waandamanaji,swali la kujiuliza je waandamanaji wangekuwa wanaandamana na silaha za moto hali ingekuwaje?