Monday, June 6, 2011

TANZANIA UMASIKINI UNATOKA WAPI?

Watanzania kadri siku zinavyozidi hali ya maisha inazidi kuwa tete,wakati hilo linatokea wanasiasa wanatuhubiria kuwa uchumi wa nchi unakua, nashindwa kuelewa uchumi unakua hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kivipi?

     Mgodi wa Ashanti uliopo katika migodi ya Geita.

             Moja ya machimbo ya madini nchini Tanzania.




Hivi karibuni katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini alitoa hotuba ambayo iliniacha mdomo wazi, katibu mkuu huyo alisema kuwa Tanzania imewekeza katika miradi mikubwa sita katika gesi,mafuta na madini, katika miradi hiyo ya madini ni mitatu ambayo uzalishaji inasemekana umeanza miaka 12 iliyopita ambapo miradi imekuwa ikiendelea vizuri sana, uzalishaji wa madini kutoka tani moja mwaka 1998 mpaka tani 50 hivi sasa unavyosoma habari hii. swali la kujiuliza kwa uzalishaji huu wa madini bado tunaendelea "kufulia" kila siku?
Wakati huo huo unaambiwa kuwa visima vya gesi vya songosongo na Mnazi bay vinatoa gesi kama upepo na huku bado kuna uwezekano mkurunga nako gesi ya kumwaga itaanza kupatikana. achilia Bahari ya Hindi na Mafia ambapo utafiti bado unaendelea. Katika hili "wadanganyika" wenzangu hatupaswi kusema kuwa Tanzania ni nchi masikini,si masikini hata kidogo labda vichwa vyetu ndio masikini. Hapo bado hatujazungumzia sekta ya utalii na rasilimali lukuki zilizotuzunguka ambazo kungekuwa na 'efficient utilization of resources' Tanzania ingeongoza kwa uchumi East Africa.