Monday, May 30, 2011

TANGAZA KUPITIA BLOG HII

BONYEZA: mobile +255 712 184 598, au +255 689 184 598
                     E-mail,   jiffjeff@yahoo.com

PICHA KALI LEO HII.

MMILIKI WA WILLIS TOWER AFANYA MAAJABU.

Mmiliki wa Jengo refu la Willis Tower lililopo Chicago nchini Marekani amejenga viboksi vya vioo vipatavyo vinne vilivyojitokeza kwa nje kwa ajili ya kubarizi uwapo katika jengo hilo. 
Jengo la Willis Tower nchini Marekani linavyoonekana kwa mbali ndani ya Chicago ambapo ghorofa ya 103 kumejengwa mabox ya vioo yaliyotokeza kwa pembeni.
Moja ya viboksi vya vioo kama unavyoona mtu anaweza kuangalia taswira ya kutisha ukiwa ghorofani.

Watoto wakila bata katika jengo la Willis Tower lililopo Chicago ndani ya Marekani.

Kama una roho nyepesi hakika hutothubutu kulala kama alivyolala mtoto huyu kutokana na ghorofa lilivyo refu.

Watalii wakipiga picha kutoka juu ghorofa ya 103.
umepaona kule chini? ni mbali sana.
Picha ikionesha jinsi unavyoweza kuingalia Chicago ukiwa ghorofa ya 103 ndani ya jengo refu la Willis Tower.

NANI KAMA MESSI.


Kwa jinsi nilivyoingalia Barcelona ni timu nzuri ambayo huwezi kuibeza hata kama una mapenzi na timu pinzani, Meneja wa Man United Sir Alex Furgerson na mchezaji wake Evra wamefunguka na kukiri hilo nami ninaungana nao kuwa Barcelona wamekuwa wazuri ndani ya miaka minne. katika kikosi cha Barcelona hakuna mchezaji wa kubeza na hili nalitamka kwani nimepata kuongea na Javier Mascherano kabla ya fainali ya jumamosi na alisema kuwa hatojisikia vibaya kama hatoanza katika mechi hiyo kwani Barcelona ina wachezaji wengi mahiri na yeye anajisijia fahari kuwa miongoni mwa kikosi hicho bora duniani. Hivyo naamini kila mchezaji ana uwezo binafsi ndani ya Barca lakini nadiriki kusema Leonnel Messi kuwa mchezaji bora wa fainali ile amestahili na ataendelea kuwa bora. staili ya uchezaji wa Messi ni kitu cha kushangaza unaweza kusema viatu vyake na mpira vinavutana ni hali ya uchezaji isiyoelezeka yaani kama uchawi vile lakini ukweli ni kwamba kipaji na mazoezi ya kujituma ndio siri ya hayo yote.

HATIMAE WAFUNGUA UKWELI WAO KUHUSU BARCELONA

Hakuna kitu kizuri kama mtu kusema kweli na kukubali mazuri ya mwenzake, mchezaji wa Man United Patrice Evra amefunguka na kukiri kuwa Barcelona wamekuwa wazuri zaidi ya miaka minne iliyopita.
Patrice Evra.
"Lazima uwapongeze Barcelona, hata kama nachezea Man na tunataka kuwa bora duniani..lakini Barcelona ni bora zaidi" anasema Evra. "Tunafahamiana lakini Barcelona wanafahamiana zaidi, kila mara Messi anajua Xavi atakua pale na Pedro atakuwa pale au Iniesta..ilikuwa mechi ngumu Barca walimiliki mpira vizuri sana" anamalizia Evra.
Kocha na meneja wa Man United Sir Alex Furgerson amefunguka na kusema kuwa Wamefungwa na timu bora japokuwa walitegemea kufanya vizuri mwisho wa siku wameambulia kipigo. "Tulitegemea kufanya vizuri lakini mwisho wa siku tukaambulia kipigo kutoka kwa timu bora" alisema Fargie.