Thursday, May 26, 2011

WANAFUNZI WENYE HASIRA WACHOMA MOTO SHULE.

                                                                     Sehemu ya mabaki ya shule hiyo baada ya huchomwa moto.
Wanafunzi wa shule ya secondary ya Amadeski Ashile Esikoleni i Sizinda ya Kwazulu Natal nchini Africa ya kusini wamechoma moto madarasa matatu ya shule hiyo kwa kile kilichoelezwa kutokuridhishwa na uongozi wa shule hiyo. Msemaji wa idara ya elimu ya Kwazulu Natal Sihle Mlotshwa ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho,pia kamanda wa polisi wa Kwazulu amesema hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo na hakuna aliyejeruhiwa na hasara iliyosababishwa na fujo hizo haikuweza kujulikana mara moja.

PICHA KALI LEO HII.

WANAFUNZI WAANDAMANA BOTSWANA BAADA YA KUTOFUNDISHWA KWA WIKI TATU.

Wanafunzi wakiwa wameweka kizuizi barabarani kupinga kutokufundishwa kwa wiki tatu baada ya walimu nchini Botswana kugomea mishahara kiduchu.

    Wanafunzi wakichoma matairi katika mgomo huo .

  Askari wa usalama wakitafuta mbinu za kukabiliana na wanafunzi.

          Mmoja kati ya wanafunzi waliogoma nchini Botswana akiwa ameketi barabarani.
           Moto ukiendelea kuwaka

      Askari wakiingia eneo la tukio kuongeza nguvu.


   Askari wa usalama wakijaribu kuzima moto uliowashwa na wanafunzi katika mgomo huo.

  Wanafunzi wanaonekana kupoteana baada ya kuzidiwa nguvu na Askari wa kutuliza ghasia.