Wednesday, May 25, 2011

ZUMA KUTEMBELEA LIBYA KWA MAZUNGUMZO NA GADDAFI

Moshi ukifuka nyuma ya mitikufuatia shambulio la anga katika eneo la Tajura
km 30 mashariki mwa Tripoli wakati majeshi ya NATO yaliposhambulia Tripolitarehe 24 mei 2011 katika harakati za kumng'oa Gaddafi.
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini anategemewa kutembelea Libya wiki ijayo, ambapo inaripotiwa kuwa safari hiyo ni maalum kwa ajili ya mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi,ambapo radio moja nchini Afrika ya Kusini Radio 702 inaripoti kuwa mazungumzo hayo yatahusu juu ya mikakati ya Gaddafi kuondoka nchini Libya. Zuma atadhuru Tripoli kwa mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi tarehe 30 mei 2011. Zuma anadhuru Libya akiwa kama kiongozi wa juu wa umoja wa Afrika katika kutatua mgogoro wa Libya, Zuma anadhuru Libya huku mwishoni mwa wiki Afrika ya kusini iliilalamikia Libya kwa kumtendea ndivyo sivyo mpiga picha wa Afrika kusini ambaye hivi sasa inaaminika kuwa amekwishakufa baada ya kupigwa risasi na askari wa Gaddafi.

ULAJI WA NYAMA HUSABABISHA UGONJWA WA KANSA.

Cut red meat intake and don't eat ham, say cancer researchers

World Cancer Research Fund advises people to limit consumption of beef, pork and lamb and avoid processed meat.
                       Beef
Eat beef with caution, the World Cancer Research Fund is advising. Photograph: joefoxfoodanddrink/Alamy
Cancer experts have issued a fresh warning about eating red and processed meat after "the most authoritative report" on the subject blamed them for causing the disease.
The World Cancer Research Fund (WCRF) is advising people to limit their intake of red meats such as beef, pork and lamb, and to avoid processed meat such as ham and salami altogether. "Convincing evidence" that both types of meat increase the risk of bowel cancer means people should think seriously about reducing how much they eat, it recommends.
The charity kickstarted a global debate in 2007 when it published a study which identified meat as a risk factor for a number of different forms of cancer.
WCRF-funded scientists at Imperial College London led by Dr Teresa Norat studied 263 research papers that have come out since then looking at the role of diet, weight and physical activity in bowel cancer. An independent panel of leading cancer experts then reviewed their conclusions. "For red and processed meat, findings of 10 new studies were added to the 14 analysed as part of the 2007 report. The panel confirmed that there is convincing evidence that both red and processed meat increase bowel cancer risk," said the report .

SHINDANO LA PICHA BORA YA MBWA NCHINI UINGEREZA LAANZA.











BAADHI YA PICHA AMBAZO TAYARI ZIMESHAKUSANYWA KATIKA SHINDANO HILO.
Unaweza kushiriki katika shindano hili unachotakiwa ni kumpiga picha mbwa akiwa mawindoni,amepumzika au picha ya juu ama pembeni na uitume.jiffjeff@yahoo.com

PICHA ZA SIKU YA KWANZA ZIARA YA OBAMA NCHINI UINGEREZA

             Obama na mkewe Michelle wakishuka katika ndege tayari kwa ziara nchini Uingereza.
Obama na Michelle wakipokelewa na Malkia.
                                                                                                                                                                               
Obama akisalimiana na wanakwaya wa Wenstiminster.
                                                                                       Obama ndani ya ikulu ya Buckingham
Obama na prince Charles wakitoka katika makazi ya balozi wa marekani kule Regent's Park.

MAN UNITED WAMSAJILI KIPA WA ATLETICO.

Kocha wa Man united ya Uingereza Sir Alex Furgeson amefunguka na kusema kuwa tayari klabu yake imeshanyaka saini ya golikipa wa Atletico Madrid ya Hispania David De Gea, De Gea anaaminika kuwa ndiye golikipa kinda ghali zaidi duniani. Mashetani hao wekundu wamemnyakua golikipa huyo kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 17 vyanzo vya habari vimeeleza.

PICHA KALI LEO HII.

Vituko vya watoto.

WENGER AFUNGUKA KWA NASRI NA CLICHY.

Wenger awachimba mkwara Nasri, Clichy

LONDON, Uingereza.
 Meneja wa Arsenal mfaransa ARSENE Wenger amewakoromea nyota wake wanaogomea kusaini mikataba mipya, Samir Nasri na Gael Clichy kwamba hatokuwa na masihara katika hilo.
Nyota hao wamebakiza mwaka mmoja katika mikataba yao na kocha huyo wa Arsenal, Wenger anataka waamue mapema kuhusu kuongeza mikataba yao au waingizwe sokoni  mwishoni mwa msimu huu.
“Tutamaliza tatizo hilo kwa haraka baada ya kumalizika kwa msimu,” alisema Wenger.
“Tunahitaji kufahamu mapema msimamo wao.”
Arsenal ilimpoteza kiungo Mathieu Flamini katika uhamisho huru mwaka 2008 baada ya kushindwa kuafikiana na nyota huyo wa Ufaransa.
Jambo hilo linamtisha Wenger na anadhani hali inaweza kujirudia.
Alisema: “Hatutaki yatokee kama yale yaliyokuwa kwa Flamini. Haturuhusu hilo kabisa. Tunataka kumaliza utata kabla ya msimu mpya kuanza.”

PIQUE AKUMBUKA MACHOZI MAN UNITED.

Pique akumbuka alivyomwaga chozi Man United


BEKI wa Barcelona, Gerard Pique, akumbushia enzi zile alipokuwa Man United na kufunguka kwamba aliwahi kumwaga machozi wakati alipokuwa akikipiga Manchester United – lakini, Jumamosi hii Mhispania huyo atakutana na United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, itakayofanyika kwenye dimba la Wembley, jijini London.
                                     Gerlard PiqueAkiwa ndani ya jezi za Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford, Pique anashukuru kwa sababu aliweza kutwaa mataji tisa na Kombe la Dunia.
Man United imebaki kuwa sehemu muhimu katika maisha yake ya soka, licha ya kwamba hakucheza mechi nyingi katika kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson, na kudai kwamba yeye binafsi ana deni kubwa la kumshukuru Mskochi huyo.
“Nilikwenda England nikiwa na miaka 17 na mambo yalikuwa magumu sana,” alisema Pique.
“Nilizoea kuwa kiwanjani katika kila mechi, lakini kwa bahati mbaya siku nyingine za mechi mimi nilikuwa nikiachwa nyumbani.
“Iliniumiza sana, na niliona sikustahili yale. Lakini, wakati ule sikuwa sawa na nilipokuwa Manchester United.
“Nilijifunza jinsi ya kukabiliana na nyakati ngumu. Nilimpigia simu mama yangu mzazi na kumweleza yote baada ya kutokwa na machozi sana.”
Pique Jumamosi hii atakuwamo ndani ya dimba wakati Barca itakapokipiga na Man United katika fainali hiyo ya Mabingwa Ulaya katika dimba la Wimbley nchini Uingereza.